Popular services

WATU WENYE ULEMAVU KIJIJI CHA CHWAKA WAOMBA KUPATIWA MSAADA WA KISHERIA.

 Watu Wenye Ulemavu wanaoishi katika Kijiji Cha Chwaka Wilaya ya Kati wameomba kuendelea kupatiwa msaada wa kisheria ili kuweza kujua haki zao.

Wakielezea changamoto zinazowakabili wakati walipokutana wanasheria wa Kituo Cha Huduma za Sheria walisema endapo elimu hiyo itawafikia mara kwa mara watakua na uwezo wa kutafuta na kuzipambania Haki zao.


Mbali na elimu ya msaada wa kisheria walisema wanahitaji kupatiwa mbinu mbalimbali zitakazowasaidia kujiunua kiuchumi.

Walieleza kuwa wanakutana na changamoto tofauti lakini wanakosa ujasiri wa kuzitafutia ufumbuzi kutokana  na kukosa gharama za mawakili na kukosa elimu ya Sheriua hivyo ZLSC imekua mkombozi kwao.


Kwa upande wake Mkurugenzi wa Kituo Cha Huduma na Sheria Felista Mauya akizungumzia kuhusu Kituo hicho alisema kipo kwa ajili ya kusaidia makundi mbalimbali  katika kujua Sheria na kupata  haki zao bila malipo likiwemo kundi la watu wenye ulemavu.

Alieleleza kupitia mradi wa.uwezeshaji kisheria unaofadhiiowa  UNDP Kituo kinatekeleza programu ya msaada wa kiSheria wa  kuhahama ili kuwafikia wananchi waliowengi

 Alifahamisha kuwa katika kutekeleza programu hiyo Zlsc itayafikia makundi yote kwa  huduma za kisheria hasa yalioyo katika  jamii ya pembezoni kwenye Shehia zote za Unguja.


Akitoa mada kwa kundi hilo mwezeshaji Dk Sikujua Omar Hamdan aliiasa jamii kuacha kuwanyanyapaa watu wenye Ulemavu jambo ambalo ni kosa kisheria.

Aidha aliwaomba wazazi na walezi wanaosimamia watoto wenye ulemavu kuhakikisha wanawasimamia vyema na kuhakikisha wanawasaidia kupata haki zao zote zinazostahili na kuwahimiza kuwa Karibu nao ili kuwakinga na vitendo vya udhalilishaji.

Hata hivyo aliwasisitiza kutumia busara na  kuwapatia ushirikiano wa kutafuta haki zao pale zinapokiukwa kwa misingi ya Sheria.


"Tunakiwa tutumie busara katika malezi yetu ili tuwakinge na majanga mbalimbali" alihimuza Dk. Sikujua

Pamoja na mambo mengine Kituo  kinajengauwelewa wa msaada kisheria ikiwemo matunzo ya watoto, migogoroya ardhi, migogoro ya ndoa na haki za watu wenye ulemavu