Popular services

MDOWE HAJI KOMBO ASISITIZA KUSIMAMIA ILANI YA CCM KWA MAENDELEO YA JIMBO LA NUNGWI

 MDOWE HAJI KOMBO ASISITIZA KUSIMAMIA ILANI YA CCM KWA MAENDELEO YA JIMBO LA NUNGWI.

Na,Nishan khamis-Fukuchani. 

Mgombea Ubunge jimbo la Nungwi kupitia chama cha mapinduzi Mdowe Haji Kombo amesema ilani ya CCM mwaka 2025-2030 imeakisi na kugusa maisha ya kila mwananchi hivyo akipata ridhaa ya kuwa mbunge jimbo hilo atahakikisha anasimamia maelekezo ta ilani kwa maendeleo ya wananchi wa jimbo hilo na maslahi ya chama na taifa kw ujumla.

Mdowe amayasema hayo hapo jana katika ufunguzi wa kampeni jimbo la Nungwi ambapo aliwaomba wananchi kuwapigia kura za ndio marais wote na viongozi wote wa CCM akiwemo yeye ili awatumikie wananchi wa jimbo hilo.