Na: Nishan Khamis, Nungwi
Jumanne, 5/08/2025.Uchaguzi wa Chama cha napinduzi nafasi za udiwani,uwakilishi na ubunge jimbo la Nungwi Wilaya ya Kaskazini “A” Unguja kwa mwaka 2025 umekamilika kwa amani na utulivu,
Msimamizi Mkuu wa Uchaguzi huo, Ramadhan Masoud Machano, alitangaza kuwa jumla ya kura za uwakilishi zilizosajiliwa ni 786 kura , kura halali 780 na kura zilizoharibika ni 6
Wagombea wa uwakilishi kwa ujumla kura zao walizopata Dkt,Salum Masoud Hamad kura 425,Ibrahim Maabad Juma kura 285,Abdalla Hamad kura 35,Abdalla Abass 18 na Hidaya Ali Makame kura 17.
Ubunge.
Jumla ya kura 787 haribika 9 Khamis Ahmada Fakih kura 334,Simai Hassan Sadik kura 349,Mdoe Haji Kombo kura 80 na Lucy John Mpembo kura15.
Udiwa wadi ya Tazari jumla ya kura 502 Halali 496,zilizo haribika 6, Twalib Haji Abas kura 309,Khamis kher Khamis kura 94 na Maryam Mtwana khatib kura 93 na udiwani wadi ya Bandakuu Khamis Vuai Lila kura 164, Simba Ali Musa kura 109 na Siti Ali Makame 36.
Washindi wa uchaguzi huo walitoa pongezi kwa wajumbe na wasimamizi wa uchaguzi pamoja na Chama Cha Mapinduzi (CCM). Waliahidi kutekeleza majukumu yao kwa bidii, uadilifu na kwa maslahi ya wanawake, chama na taifa kwa ujumla.
Wajumbe walioshiriki uchaguzi huo walieleza kuridhishwa kwao na uendeshaji wa uchaguzi huo kwa haki, uwazi na utulivu. Walihimiza viongozi waliochaguliwa kutumia nafasi walizopewa katika kushughulikia changamoto mbalimbali na kuendeleza ustawi wa wanawake na jamii kwa ujumla.
