Popular services

MWENYEKITI CCM JIMBO LA NUNGWI AWAOMBEA KURA ZA NDIO DKT SAMIA, DKT MWINYI, WABUNGE, WAKILISHI NA MADIWANI.

 Na,Nishan khamis. 

jumatano,17-09-2025 Nungwi.

Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Nungwi, Ali Mtwana maarufu Kabila, amewaomba wananchi wa jimbo hilo na Watanzania kwa ujumla kujitokeza kwa wingi Oktoba 29 mwaka huu na kuwapa kura za ndiyo wagombea wa CCM, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Samia Suluhu Hassan, Rais wa Zanzibar Dkt. Hussein Ali Mwinyi, pamoja na wabunge, wawakilishi na madiwani wote wa CCM.

Aidha, Kabila amewahimiza wanachama na wapenzi wa chama hicho kujitokeza kwa wingi kesho katika mapokezi ya Mwenyekiti wa CCM Taifa yatakayofanyika huko Nungwi, akisisitiza kuwa mapokezi hayo ni fursa ya kuonesha mshikamano na mshikamanisho wa chama kuelekea uchaguzi mkuu.


Akizungumza leo na mwandishi wa habari hizi kuhusu maandalizi ya mapokezi hayo, Mtwana amewataka wana CCM na wananchi kwa ujumla kuendelea kudumisha amani na utulivu hasa katika kipindi hiki cha uchaguzi mkuu nchini, akibainisha kuwa CCM itaendelea kuwa mstari wa mbele katika kulinda mshikamano wa kitaifa.