Mgombea wa Nafasi ya Urais wa Zanzibar, kupitia Chama cha ACT-Wazalendo, ambaye pia ni Makamu wa Kwanza wa Rais, Mheshimiwa Othman Masoud Othman, Leo September 16, 2025, ameendelea na Kampeni, kwa kukhutubia Mkutano ya Hadhara wa Chama hicho, uliofanyika katika Viwanja vya Skuli ya Makangale, Jimbo la Konde, Wilaya ya Micheweni, Mkoa wa Kaskazini Pemba.
Mheshimiwa Othman ambaye ni Mwenyekiti wa Taifa wa Chama hicho, amepata fursa ya kuwaomba wananchi kura za ndiyo, ili apate ridhaa ya kuongoza Serikali ya Zanzibar, ambapo pia amewanadi na kuwaombea kura wagombea wa nafasi za Ubunge, Uwakilishi na Udiwani katika jimbo hilo.
Kitengo cha Habari
Ofisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar
Septemba 16, 2025.


