Alhamisi 4,09-2025.
Mkuu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja ambaye pia ni Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama mkoa huo, Mhe. Mattar Zahor Masoud, amewataka watu wenye ulemavu kutokuwa na hofu katika kushiriki uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba mwaka huu.
Akizungumza katika kongamano la watu wenye ulemavu lililofanyika Chuo cha Amali Mkokotoni, Wilaya ya Kaskazini A, kwa niaba ya Mkuu wa Mkoa, Bi. Mboja Hesabu Ali alisema serikali ya mkoa imeweka mazingira na huduma rafiki kwa watu wenye mahitaji maalumu katika kampeni na vituo vya kupigia kura ili kuhakikisha wanatimiza haki yao ya msingi ya kikatiba.
Bi. Mboja alisisitiza kuwa serikali ya mkoa imejipanga kuhakikisha amani na utulivu vinatawala kabla na baada ya uchaguzi. “Tunataka kila mwananchi ajisikie salama kushiriki uchaguzi, bila hofu wala wasiwasi, ili demokrasia iendelee kustawi,” alisema.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa Baraza la wWatu Wenye Ulemavu Zanzibar, Bi Salma Saadati Haji, aliwahamasisha watu wenye mahitaji maalum kujitokeza kushiriki si tu kupiga kura, bali pia kugombea nafasi za uongozi. “Ni wakati sasa wa sisi wenye ulemavu kuonyesha uwezo wetu katika nafasi za uongozi, kwani uwazi na ushiriki ni haki ya kila mmoja wetu,” alisema.
Washiriki wa kongamano hilo walieleza changamoto wanazokumbana nazo, ikiwemo mazingira magumu ya kushiriki upigaji kura, na wakaomba serikali pamoja na vyama vya siasa kuimarisha msaada wa mazingira rafiki ili kuhakikisha wanatimiza haki yao ya kidemokrasia bila vikwazo.
Kongamano hilo ambalo limehudhuriwa na watu wenye mahitaji maalum kutoka mikoa yote ya Zanzibar, lilibeba kauli mbiu isemayo: “Haki za watu wenye ulemavu ni haki za binadamu — hakikisha ushiriki wa watu wenye ulemavu katika siasa na uongozi.” Kongamano hilo pia limekuwa sehemu ya Kongamano la 2025 la Wadau wa Maendeleo Jumuishi katika Jamii, na limeandaliwa na Shirikisho la Jumuiya za Watu Wenye Ulemavu Zanzibar (SHIJUWAZA).