Popular services

WAGOMBEA CCM JIMBO LA NUNGWI WAAHIDI KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA WANANCHI ✅


Na,Nishan khamis-Kigunda.

Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa(MNEC) Ndugu Amin Salmin Amour amesema rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Husein Ali ametekeleza kwa vitendo ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025 kutokana na kuimarisha miundoni mbali mbali katika nyanza zote jambo amabalo limevutia ongezeko la Utalii katika kijiji cha Nungwi na Zanzibar kwa ujumla.

Amesema hayo hapo jana katika uwanja wa mpira wa Shehia ya kigunda , jimbo la Nungwi, Wilaya ya Kaskazini A, wakati wa mkutano wa hadhara uliohudhuriwa na wanachama na wananchi mbalimbali, ikiwa ni mwendelezo wa kampeni za chama cha mapinduzi katika jimbo hilo.

Ameeleza kuwa  chama hicho kinaendeshwa na kanuni na taratibu hivyo umoja wao ni silaha kwa wana ccm kuendelea kukipatia ushindi wa kishindo hicho huku amewaeleza kuwa Dkt Mwinyi ni mtekelezaji wa ilani kwa vitendo jambo ambalo limekuza utali na sekta mbali mbali nchini jambo ambalo wana kila sababu ya kuunga mkono juhudi za kimaendeleo kwa kumpa kura za ndio ifikapo Oktoba 29 siku ya uchaguzi ili aendelee kuleta maendeleo zaidi nchini.

Aidha amesisitiza wasiadaiwe na wenye nia mbaya na maendeleo ya yanayo fanywa na Dkt Husein Ali Mwinyi pamoja na Dkt Samia Suluhu Hassan bali waendelee kuwaunga mkoa viongozi hao na kuwapa kura za ndio viongozi wote wa CCM nchini ili ilani ya CCM 2025-2030 itimize zaidi maendeleo ya vitendo nchini.

Kwa upande wao, wagombea wa nafasi mbalimbali jimboni humo walisema kuwa kupitia Ilani ya CCM ya mwaka 2020-2025, chama kimefanikisha utekelezaji wa miradi ya maendeleo kwa zaidi ya asilimia 100, ikiwemo sekta za miundombinu ya barabara, elimu, afya, kilimo, michezo na uwezeshaji wa mikopo kwa wajasiriamali na wanafunzi wa vyuo. Walimpongeza Rais Dk. Hussein Ali Mwinyi kwa jitihada kubwa za maendeleo.

Wagombea hao walisisitiza kuwa endapo watapewa ridhaa tena, wataendeleza kusimamia  utekelezaji wa Ilani ya CCM ya mwaka 2025-2030  kwa kusimamia changamoto za shehia za kigunda zikiwemo barabara za ndani,maji,elimu,pensheni kwa wazee pamoja kutumia fursa ya utalii kwenye jimbo hilo ili kuzalisha ajira kwa vijana.

Aidha wamesisiza wananchi kuendelea kushirikiana nao,kutunza amani na utulivu na kujitokeza kwa wingi siku ya kupiga kura na kuwachagua viongozi wote wa CCM ili kuendeleza maendeleo katika jimbo hilo.

Baadhi ya wanachama waliohudhuria mkutano huo walisema hali ya kisiasa jimbo ni salama huku wakiridhishwa na utekelezaji wa maendeleo katika jimbo lao, na wakaahidi kulipa fadhila kwa chama hicho kwa kura za ndiyo ifikapo tarehe 29 Oktoba pamoja na kuendeleaza kutunza amani na utulivu nchini.