Popular services

DKT SALUM:NITASIMAMIA CHANGAMOTO JIMBO LA NUNGWI KATIKA NYANZA ZOTE, AOMBA USHIRIKIANO.

 Na,Nishan khamis. 

Mgombea uwakilishi jimbo la Nungwi Kupitia Chama Cha Mapinduzi Dkt Salum Soud amesema endapo atapata ridhaa ya kuchaguliwa kuwa mwakilishi jimbo hilo atahakikisha anasimamia changamoto zote katika elimu, afya,kijamii na kiuchumi ili kupeleka mbele maendeleo ya jimbo hilo.


Dkt Salum aliyasema hayo hapo jana katika uzinduzi wa kampeni jimbo la Nungwi hivyo aliomba ushirikiano kwa wananchi kwa kuwpa kura za ndio marais wote wa CCM nchini na viongozi wote wa CCM wa jimbo hilo na kujiombee yeye ili kuja kusimamia maendeleo zaidi katika jimbo hilo.