Na,Nishan khamis Pemba
Mbunge wa Jimbo la Mkoani Pemba ambaye waziri wa ujenzi na Uchukuzi Mhe, Profesa Makame Mbarawa jana ameendelea kutekeleza ahadi zake kwa wanafunzi wa jimbo lake walio faulu michipuo wapata 140 kwa kuwwakabidhi mikoba badala ya awali kuwakabidhi magodoro na sare za skuli.
Profesa Mbarawa ameyasema hayo jana nyumbani kwake Mkanygeni wakati akizungumza na wazazi pamoja wanafunzi waliofaulu michipuo jimbo hilo katika hafla ya kukabidhi mabegi ya kisasa kwa wanafunzi hao.
Amesema kitendo hicho ni utekelezaji wa ilani ya CCM kwa vitendo kwani serikali ya mapinduzi ya Zanzibar inayoongozwa na Dkt Husein Ali Mwinyi na serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania inayoongozwa na Dkt Samia Suluhu Hassan imeimarisha miundombinu ya elimu bora na inaendelea kuimarisha ziadi ikiwa na azma bora kwa maendeleo ya wanafunzi nchini kwa kuwaandaa vijana hao kuwa wasomi bora kwa maendeleo ya badae kwa jamii na taifa kwa ujumla.
Halikadhalika Mheshimiwa Mbarawa aliwakabidhi wananchi wa jimbo hilo mipira ya maji na matanki ya maji jimbo zima ili kutatua changamoto za ukosefu wa vifaa hivyo ili waweze kupata maji safi na salama kwa maslahi mapana ya kiafya kwa jamii.
Aidha amesema jumla ya shilingi milioni ishirini imetumika katika ununuzi wa vifaa kwa wanafunzi na shilingi milioni thelathini zimetumika katika kununulia mipira ya maji na matanki ya maji na amewahakikishia ataendelea kushirikiana nao katika harakati zote za kutatua changamoto jimbo hilo na kupeleka mbele maendeleo chanya.
Profesa Mbarawa ametoa wito kwa wanafunzi hao kusoma kwa bidii ili kufanikisha ndoto zao sambamba na kuwaomba wazazi kuwahudumia watoto hao na kutunza miundombinu ya maji ili itumike kwa muda mrefu zaidi ili kuepukana na changamoto ya maji katika jimbo hilo.
Awali akizungumza katika hafla hiyo mwenyekiti wa CCM jimbo la mkoa Omar Ngwali Dadi,amempongeza Mheshimiwa mbunge kwa utekelezaji wake wa vitendo na ishara nzuri ya kuitendea haki ilani ya chama hicho kwa utekelezaji wa vitendo kwa wananchi kwani mikoba iyo itakuwa ni chachu ya kufanya vyema wanafunzi hao sambamba na utoaji wa mipira ya maji na matanki ni suala la kupongezwa kwa jitihada kubwa anazo zifanya katika jimbo hilo.
Kwa upande wake mwakilishi wa viti maalum mkoa huo Maryam Said Khamis amewanasihi wanafunzi hao kusoma kwa bidiii na kuto jihusisha katika vitendi vya ushawishi ambavyo vitapelekea kukatish ndoto zao bali wafanye juhudi za kusoma kwa bidii na nidhamu ili watimize ndoto zao.
Nao wanafunzi wamesema wamefurahishwa na zawadi izo na kushukuru kwa hamasa hiyo na wameahdi kuyachukua na kuyafanyia kazi yale yote waliyo ambiwa na upande wa wananchi wamesema watahakikisha vifaa vya maji wanasimamia na kutunza miundombinu iyo ili idume kwa muda mrefu zaidi kwa maendeleo endelevu jimbo hilo..


