Popular services

HAZINA CLUB YA MKWAJUNI WASHIKA NAFASI YA PILI, WAMPONGEZA DIWANI UNJU KWA HAMASA YAKE.

 

Na Nishan Khamis Mkwajuni
Diwani wa Wadi ya Kidombo, Makame Machano Fumu, maarufu Unju, amewapongeza vijana wa Hazina Club kwa kuibuka wa pili katika mashindano ya riadha ya Mapinduzi Cup mwaka 2026.

Diwani Unju amesema mafanikio hayo yanatokana na juhudi za wachezaji na sapoti ya viongozi, na kuwataka kuendelea kufanya vizuri sambamba na kutunza amani na utulivu, kwani hizi ni tunu na matunda ya maendeleo nchini.

Pia alisisitiza umuhimu wa michezo kama fursa ya ajira, afya na heshima ya wadi.
Kwa upande wake, Makame Khatib Haji, mwenyekiti wa Hazina Club, amesema motisha waliyoipata kutoka kwa diwani imewafanya wachezaji kuendelea kufanya vizuri na kuhakikisha katika mashindano yajayo wanashiriki kwa ubora, ili kuleta ushindi na medali nyingi zaidi kwa wadi hiyo. Pia ametoa pongezi kwa diwani na kumuomba kuendelea kuwaunga mkono, kwani licha ya mafanikio bado kuna changamoto zinazowakabili.

Katibu wa riadha wa club hiyo, Ali Mtuma, ameeleza kuwa jitihada na sapoti ya diwani zimewapa hamasa kubwa, na amempongeza diwani Unju kwa kuendelea kuwaunga mkono wanachama wa club hiyo, huku wakihamasishwa kuendeleza mafanikio na kufanya vyema katika mashindano yajayo.