Popular services

YUMNA,MGOMBEA UWAKILISHI JIMBO LA CHAMBANI AHAIDI KUSHUGHULIKIA CHANGAMOTO ZA WANANCHI, AOMBA KURA ZA NDIO OKTOBA 29.

 

Na,Nishan khamis-Mapepe Chambani.
Mgombea wa uwakilishi Jimbo la Chambani kupitia chama cha ADA–TADEA Yumna Ahmed Khalid, jana alifanya mkutano na wananchi wa Kijiji cha Mapepe ambapo aliwasikiliza na kujadiliana nao kuhusu changamoto zinazowakabili, ikiwemo upatikanaji wa maji safi na salama, huduma za afya, miundombinu ya barabara na ajira kwa vijana.

Akizungumza katika mkutano huo, mgombea huyo aliahidi kuwa atashirikiana kwa karibu na serikali itakayokuwa madarakani ili kuhakikisha changamoto hizo zinapatiwa ufumbuzi wa kudumu. Alitoa wito kwa wananchi wa Chambani kumpa kura za ndiyo ifikapo Oktoba 29, akisisitiza umuhimu wa kudumisha amani na utulivu katika kipindi chote cha kampeni na uchaguzi.

Yumna, amewahimiza vijana wenzake kumpa sapoti ili kuibadilisha Chambani kuwa jimbo la kimaendeleo zaidi, lenye fursa sawa kwa wananchi wote pamoja na kuwa mstari wa mbele vijana katika kuhubiri na kutunza amani na utulivu kabla na baada ya uchaguzi.

Kwa upande wake, mama yake mgombea huyo, Asha Said Suleiman, amesema atahakikisha yuko pamoja naye na kumsaidia mwanaye kufikia malengo yake ya kisiasa na uongozi kwa maslahi ya wananchi wa Chambani, hasa wanawake, watoto, vijana na wazee. Ametiab wito kwa jamii kumchagua kijana huyo ili kuonesha kuwa wanawake ni watu wa maendeleo wanapoungwa mkono.

Baadhi ya wananchi waliohudhuria mkutano huo walionesha kufurahishwa na uthubutu na misimamo ya mgombea huyo, wakisema sera zake zina mvuto mkubwa na zinaashiria mabadiliko chanya katika maendeleo ya jimbo hilo,hivyo wameahid kumpa kura za ndiyo ifikapo Oktoba 29.