Popular services

DKT MWINYI:AHIDI TUMBATU KUWA WILAYA KAMILI.

 Mgombea nafasi ya Urais wa Zanzibar kupitia tiketi ya Chama Cha Mapinduzi(CCM), Dk.Hussein Ali Mwinyi amewaahidi wananchi wa kisiwa cha Tumbatu katika miaka mitano ijayo atahakikisha anaifanya kisiwa hicho kuwa wilaya.

Kauli hiyo ameitoa wakati akizungumza katika mkutano wa kampeni unaofanyika kisiwa cha Tumbatu kilichopo wilaya ya Kaskazini ‘A’ mkoa wa Kaskazini Unguja.

Dk.Mwinyi amesema kuna wakati wakazi wa kisiwa cha Tumbatu walimuomba kuifanya kisiwa hicho kidogo kuwa wilaya kamili na kwamba anawahakikishia ataifanya hivyo kipindi kijacho.

“Sasa ni wakati Tumbatu kuwa wilaya kamili kuna kipindi tuliitaka wizara husika waanze mchakato wakulifikisha hilo wakaniambia kuna vigezo lazima vitimie na kwamba ahaadi yenu kwenu ni kipindi kijacho tutaongeza wilaya na kuifanya iwe wilaya kamili,”amesema