Popular services

 Rahma Khamis Maelezo 

Mkurugenzi Mtendaji Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa Zanzibar Makame Khatib Makame amezitaka Taasisi za Serikali na Wizara mbalimbali kushirikiana katika kuwekeza kifedha ili kukabiliana na athari za Maafa nchini

Ameyasema hayo huko Chuini Wilaya ya Magharibi A' katika Kilele Cha maadhimisho ya Kimataifa ya kupunguza Athari za Maafa Duniani.


Aidha amezitaka Taasisi hizo kushirikiana na wananchi katika kupambana na Maafa ili kujikinga na majanga mbalimbali.

Amesema kuwa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa imeadhimisho hiyo kwa kufanya upimaji wa afya bure wa maradhi mbalimbali kwa wananchi  ili kujenga uhimilivu kwa jamii na kuwanusuru na Maafa yatokanayo na maradhi.

Amefahamisha kuwa wananchi wanakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwemo maradhi hivyo kufanya hivyo kutasaidia kujua matatizo yao na kupatiwa ufumbuzi

"Tukijenga afya ya leo tutawekeza kesho na kujikinga na majanga" alisema Mkurugenzi Khatib

Akizungumzia kuhusu Uchaguzi Mkuu unayotarajiwa kufanyika Oktoba 25 mwaka huu amewataka wananchi  kupiga kura kwa Amani ili kujikinga na athari za majanga zinazoweza kukjitokeza kutokana na vurugu.

Mkurugenzi wa Manispaa Magharibi A' Mhamed Simba Hassan ameushukuru Uongozi wa Kamisheni ya Kukabiliana na Maafa kwa kiwasogezea huduma za upimaji wa afya karibu bila ya Malipo.

Aidha amewaasa wananchi kuepuka kujenga katika maeneo yenye mambonde na  kutuama  maji ili kujikinga na athari za Maafa sambamba na kuacha kuchukua vitu vitakavyosababisha Maafa wakati watakapokwenda kupiga kura ili kuzuwia  maafa wakati wa vurugu likitokea.

Mratibu Msaidizi wa huduma za Afya ya Jamii kutoka Wizara ya Afya  Ali Haji Simai amesema kuwa wananchi wamehamasika kujitokeza kwa wingi na kuwataka kuendelea kujitokeza ili kupata huduma na matibabu.

Nao wananchi waliyojitokeza kupima wamesifu huduma zilizotolewa na kuwaomba wananchi wenzao kujitokeza ili kujua afya zao.

Katika Maadhimisho hayo upimaji wa maradhi mbalimbali umefanyika ikiwemo Saratani ya Matiti, Shingo ya kizazi, homa ya Ini, Kifua Kikuu, Utoaji wa damu Sukari na presha.