Na, Nishan Khamis – Mkwajuni
Mwenyekiti wa Kamati ya Bodi ya Hospitali ya Wilaya ya Kivunge ambaye pia ni Sheha wa Shehia ya Mkwajuni, Jumbe Iddi Jumbe, amewataka wamama wajawazito kujitokeza kwa wingi na kwa wakati kufika kliniki ili kuepusha vifo vya mama na watoto vinavyoweza kuepukika.
Sheha Jumbe alitoa wito huo katika kikao kilichofanyika mtaa wa Uyagu wakati akizungumza na wakazi wa Shehia ya Mkwajuni, Wilaya ya Kaskazini A, Mkoa wa Kaskazini Unguja. Amesema bado kuna idadi ndogo ya wamama wajawazito wanaohudhuria kliniki kwa wakati, jambo linaloweza kusababisha changamoto kubwa za kiafya kwa mama na mtoto.
Amefafanua kuwa ni jukumu la wanaume pia kuhamasisha wake zao kutambua umuhimu wa kuhudhuria kliniki mapema, ili kuhakikisha afya bora kwa mama na mtoto na kuepusha vifo vya kizembe.
Kwa upande wao, baadhi ya wanawake waliohudhuria kikao hicho wamesema licha ya Serikali ya Awamu ya Nane inayoongozwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi, Dk. Hussein Ali Mwinyi, kuboresha huduma za afya, bado kuna changamoto ya kukaa muda mrefu kusubiri huduma wanapofika hospitalini.
Wameiomba serikali kuhakikisha wamama wajawazito wanapewa kipaumbele wanapofika kliniki, ili kuepusha usumbufu na ucheleweshaji wa huduma.
Katika kikao hicho, mmoja wa wazee waliohudhuria, Adam Mlekwa, aliwataka wanawake kuwa mstari wa mbele kuhamasisha amani na utulivu nchini, pamoja na kujitokeza kwa wingi kushiriki uchaguzi mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 m
