Na,Nishan khamis-Kidoti.
Mjumbe wa Halmashauri Kuu ya CCM Taifa, Ndugu Amin Salmin Amour, ambaye pia ni Msimamizi wa Uchaguzi wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Jimbo la Nungwi, amewahakikishia wananchi wa Kidoti na Jimbo la Nungwi kwa ujumla kwamba amani na utulivu vitatawala kabla na baada ya Uchaguzi Mkuu unaotarajiwa kufanyika Oktoba 29 mwaka huu.Ndugu Amin aliyasema hayo leo katika Kijiji cha Kidoti, alipokuwa akiendelea na kampeni ya “Amka Nungwi Kumekucha”, yenye lengo la kuwatembelea waasisi wa Mapinduzi, wanachama wa CCM, wagonjwa, na kushiriki katika upandishaji wa bendera kwa mabalozi wote wa jimbo hilo. Kampeni hiyo pia inalenga kuhamasisha jamii kuhusu umuhimu wa kudumisha amani na utulivu, pamoja na kukiombea kura Chama Cha Mapinduzi siku ya uchaguzi.
Amesema kuwa, kama msimamizi wa chama katika jimbo hilo, atahakikisha amani na utulivu vinatawala kipindi chote cha uchaguzi, kwani CCM ndicho chama pekee kinachohubiri amani na utulivu nchini. Amewataka wazazi, walezi na vijana kushirikiana katika kudumisha hali hiyo na kuepuka vitendo vyovyote vinavyoweza kusababisha uvunjifu wa amani, huku akisisitiza kufuata kanuni na sheria za nchi kwa misingi ya kuimarisha maendeleo.
Aidha, Ndugu Amin amewahimiza wananchi wa Jimbo la Nungwi kukiunga mkono Chama Cha Mapinduzi kutokana na maendeleo makubwa yaliyopatikana, ikiwemo uimarishaji wa miundombinu mbalimbali. Ameomba ifikapo Oktoba 29, wananchi watoe kura za ndio kwa CCM ili kuendeleza maendeleo nchini.
Kwa upande wake, Mwenyekiti wa CCM Jimbo la Nungwi, Ndugu Ali Habibu Mtwana, amesema hali ya kisiasa katika jimbo hilo ni shwari, na wameendelea kuhimiza wananchi kutunza amani. Ameomba wananchi kujitokeza kwa wingi siku ya uchaguzi kwa utulivu na amani, na kuichagua CCM katika ngazi zote, ili kuhakikisha Ilani ya CCM 2025–2030 inatekelezwa kwa manufaa ya maendeleo zaidi jimboni humo.
Baadhi ya wananchi walioshiriki katika ziara hiyo wamesema wamefurahishwa na kampeni hiyo, wakieleza kuwa imewaongeza hamasa kuelekea uchaguzi mkuu. Wameahidi kudumisha amani na utulivu kabla na baada ya uchaguzi, pamoja na kujitoa kwa wingi siku ya kupiga kura kuichagua CCM. Hata hivyo, wameomba tatizo la maji na uwezeshaji wa kiuchumi kwa wananchi wa jimbo hilo kushughulikiwe ipasavyo.
Ziara hiyo ya siku tatu leo ilimtembelea miongoni mwa waasisi 12 wa mapinduzi kidoti mzee Sheha Haji Khamis na bi Miza Ndende Juma miongoni mwa waasisi CCM Kidoti na Jumla ya mabalozi tisini na tisa wametembelewa na kupachikiwa bandera za chama cha mapinduzi na kuangalia idadi ya wanachama wa CCM jimbo hilo ikiwa ni shamra shamra kuelekea uchaguzi mkuu Oktoba 29.


