Na Nishan Khamis
Diwani wa Wadi ya Kidombo, Makame Machano Fumu, maarufu kwa jina la Unju, amewataka wanakijiji wa Njaro kushirikiana kwa pamoja katika kuchimba kisima ili kumaliza changamoto ya upatikanaji wa maji inayowakabili kwa muda mrefu.Diwani huyo ameyasema hayo katika kikao chake na wananchi wa kijiji cha Njaro kilichopo ndani ya Wadi ya Kidombo, ambapo wananchi walieleza malalamiko yao kuhusu uhaba wa maji safi na salama, hali inayosababisha usumbufu mkubwa katika shughuli zao za kila siku.
Wananchi hao wamesema tatizo hilo limekuwa likijirudia mara kwa mara na kuathiri maisha yao ya kijamii na kiuchumi, huku baadhi wakilazimika kutembea umbali mrefu kutafuta huduma ya maji.
Akijibu hoja hizo, Diwani Unju amesisitiza umuhimu wa ushirikiano baina ya viongozi na wananchi katika kutafuta suluhisho la kudumu. Amesema kuchimba kisima ni moja ya hatua za haraka na za msingi zitakazosaidia kupunguza changamoto hiyo kwa kiasi kikubwa.
Ameongeza kuwa yupo tayari kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo ili kuhakikisha mradi huo unatekelezwa kwa mafanikio, huku akisisitiza kuwa mshikamano wa wananchi ni nguzo muhimu katika kufanikisha azma hiyo.
Kwa upande wao, baadhi ya wanakijiji wameeleza kufurahishwa na juhudi za Diwani huyo kwa kipindi kifupi tangu aingie madarakani, wakisema ameonesha dhamira ya dhati katika kusikiliza na kushughulikia changamoto za wananchi. Wamempongeza kwa mchango wake na kuahidi kuendelea kumpa ushirikiano katika kuwaletea maendeleo ya kijiji cha
