Popular services

 Mwandishi: Nishan Khamis

Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Tanzania ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Chaani, Mhe. Ayoub Mohammed Mahmoud, amewatuma wahandisi maalum kufanya ziara katika skuli na vituo vya afya vya jimbo hilo kwa lengo la kukusanya taarifa za mahitaji na changamoto zinazohitaji ufumbuzi wa haraka.

Wahandisi hao Zakaria na Abdulson Ali Gamesa walitembelea baadhi ya skuli na vituo vya afya na kukusanya taarifa kutoka kwa viongozi wa taasisi hizo kuhusu hali ya utoaji wa huduma na maeneo yanayohitaji kuboreshwa.

wamesema hatua hiyo ni sehemu ya utekelezaji wa dhamira ya kuhakikisha maendeleo ya haraka yanawafikia wananchi kupitia mpango wa “Chaani Mpya kwa Wote”, unaolenga kuboresha huduma za elimu na afya kwa wananchi.

Diwani wa Wadi ya Chaani, Khamis Haji Ali, alisema ziara hiyo inalenga kuweka mkakati wa pamoja wa kutatua changamoto za wananchi kwa hatua za haraka na endelevu.