Popular services

MHE. SHADYA AWAFARIJI WANAWAKE WENYE MAZINGIRA MAGUMU KASKAZINI UNGUJA KWA SADAKA YA IFTAR.

 MHE. SHADYA AWAFARIJI WANAWAKE WENYE MAZINGIRA MAGUMU KASKAZINI UNGUJA KWA SADAKA YA IFTAR.

Na,Nishan khamis, Zanzibar. 

Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mhe. Shadya Haji Omar, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Khashama Foundation, amefanya ziara ya kuwatembelea wanawake wajane, wanaoishi katika mazingira magumu pamoja na wazee, kwa lengo la kuwafariji na kuwapatia sadaka ya iftar ili kuwasaidia katika Mfungo Mtukufu wa Ramadhani.

Akizungumza wakati wa ziara hiy, Mhe. Shadya amesema hatua hiyo ni sehemu ya jitihada zake za kuendelea kuwatembelea na kuwa karibu na wanawake wanaoishi katika mazingira hayo, ili kuonesha mshikamano na ushirikiano wa dhati kati yake na wananchi anaowawakilisha, hasa wanawake wa Mkoa wa Kaskazini Unguja sadaka zilizo tolewa ni ngano kila 5,sukari kilo 5,mafuta,tende na maharage. 

Aidha, ametoa wito kwa viongozi wengine kuiga mwenendo wa viongozi wakuu wa nchi, akiwemo Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan pamoja na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Hussein Ali Mwinyi, katika kuwatumikia wananchi kwa moyo wa kujitolea na kuwajali.

Kwa upande wao, wananchi waliotembelewa na Mheshimiwa Mbunge wameeleza shukrani zao za dhati kwa moyo wa upendo na kujali unaooneshwa na kiongozi huyo. Wamesema msaada huo umewafariji na kuwasaidia katika kipindi hiki cha Mfungo wa Ramadhani, huku wakitoa wito kwa viongozi wengine kuiga mfano huo wa kuwajali wananchi, hususan wale wanaoishi katika mazingira magumu.