Popular services

MBUNGE SHADYA AWAPA FARAJA AKINA MAMA WALIYOJIFUNGUA HOSPITALI YA KIVUNGE KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

 MBUNGE SHADYA AWAPA FARAJA AKINA MAMA WALIYOJIFUNGUA HOSPITALI YA KIVUNGE KATIKA MAADHIMISHO YA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI.

Na,Nishan khamis,Zanzibar
Mbunge wa Viti Maalum Mkoa wa Kaskazini Unguja, Mhe. Shadya Haji Omar, ambaye pia ni Mkurugenzi wa Taasisi ya Khashama Foundation, amewasisitiza wazazi na walezi kuwa makini katika malezi ya watoto ili kuwajenga katika maadili mema na kuwaepusha na mazingira hatarishi yanayoweza kusababisha vitendo vya udhalilishaji.

Mhe. Shadya ametoa kauli hiyo leo alipofanya ziara ya kuwatembelea na kuwajulia hali akina mama waliojifungua katika Hospitali ya Wilaya ya Kivunge. Amesema kuwa kwa kuwa leo ni maadhimisho ya wanawake Duniani, ameona umuhimu wa kuungana na wanawake hao kwa kuonesha nafasi na mchango mkubwa wa mwanamke katika jamii.

Aidha, amewahimiza wanawake kuwa mstari wa mbele katika malezi ya watoto, akieleza kuwa wao ndio wenye jukumu kubwa la kuwalea katika misingi ya maadili. Katika ziara hiyo, Mheshimiwa Shadya pia alitoa msaada wa sabuni na pampasi kwa ajili ya kuwasaidia akina mama hao katika matumizi ya kila siku, huku akiahidi kuendelea kuwa karibu nao katika harakati mbalimbali za maendeleo katika mkoa huo.

Kwa upande wake, Daktari wa zamu katika wodi ya wazazi katika Hospitali ya Kivunge, Mohammad Suleiman Ali, amempongeza Mheshimiwa Mbunge kwa ziara hiyo ya kuwajulia hali akina mama waliojifungua, akisema kuwa hatua hiyo inaleta faraja kubwa kwa wagonjwa pamoja na watumishi wa afya, huku akibainisha kuwa msaada uliotolewa una umuhimu mkubwa kwa akina mama hao.

Naye Halima Hussein Fomu, mmoja wa wanawake waliojifungua katika hospitali hiyo, ametoa shukrani zake za dhati kwa Mheshimiwa Mbunge kwa kuwajali na kuwafariji. Amesema ujio wa viongozi kama hao hospitalini unawatia moyo na kuwapa faraja, na kuwataka viongozi wengine kuiga utamaduni huo wa kuwajulia hali wananch