Popular services

 Na,Nishan khamis. Kaskazini Unguja.

Tarehe 15.April 2026.
Taasisi ya ZIC Takaful kwa kushirikiana na jumuiya ya kusaidia wanafunzi mkoa wa kaskazini Unguja(JUKWAMKU)  leo wametoa msaada wa vifaa vya skuli kwa mayatima 30 ikiwa ni sehemu ya malengo ya jumuiya katika kusaidia wanafunzi na jamii kwa ujumla.

Akizungumza katika hafla iyo uko kitope wilaya ya kaskazini B Kaimu mkurungezi mwendeshaji wa ZIC Said Basleym amesema lengo na taasisi iyo kusimami utoaji wa huduma za kijamii kwa kusadia na kushiriki katika maswla mabli mbali ya kijamii kama taasisi ya serikali wapo katika jitihada izo za kupeleka mbele maendeleo ya kijamii kwa maslahi mapana ya jamii na taifa kwa ujumla.

Aidha ametoa pongezi kwa kwa jumuiya ya JUKWAMKU kwa jitihada za kuendelea kusaidi jamii na amewahakikishia kuendelea kushirikiana nao katika kuleta maendeleo ya jamii nchini.

Wakizungumza katika hafla iyo mwenyekiti wa JUKWAMKU Ali Abdulla Ali na katibu wa jumuiya hiyo Soud Omar khamis wamesema jumuiya imejikita zaidi kutoa misaada ya kibinadamu  ya kijamii ya kidini kwa kutoa vifaa vya skuli ,kuchimba visimba na harakati mbalimbali za kijamii.

Wamesema katika kuendeleza harakati zao wametoa pongezi za dhati kwa taasisi ya ZIC kwa kuwaunga mkono na kujumuika kwa pamoja katika kuwapatia watoto thelathini mayatima vifaa vya skuli ikiwa ni sehemu ya utekelezaji wa majukumu yao katika taasisi, hivyo ameiomba taasisi hiyo kuendelea kushirikiana nao katika utatuzi wa changamoto mbali mbali za kijamii.
Nao wazazi w

Nao wazazi Aziza Issa Mohammed  na Yussuf Thani Amour, waliohudhuria katika hafla iyo wmaetoa shukrn za dhati kwa taasisi izo kwa msaada huo na kuwaomba isiwe mwisho katika harakati muhimu za kuisaidia jamii.