MARYAM SAID KHAMIS AAPISHWA BUNGENI DODOMA, AINGIA RASMI KWENYE UWAKILISHI WA KITAIFA
Na,Nishan khamis,Mhe. Maryam Said Khamis ni miongoni mwa wabunge wateule sita waliokula kiapo cha uaminifu na uzalendo leo katika Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jijini Dodoma.
Maryam, ambaye ni Mwakilishi wa viti maalum kutoka Mkoa wa Kusini Pemba, ameingia rasmi katika nafasi hiyo baada ya kuhudumu kama Katibu Tawala wa Wilaya ya Kaskazini A, Unguja.
Tukio hili linaashiria hatua muhimu katika safari yake ya uongozi na uwakilishi wa wananchi wa Zanzibar katika Bunge la Jamhuri ya Muungano.
