Jumatatu, 4/08/2025.
Zoezi la kupiga kura kwa wajumbe wa CCM kwa ajili ya kuwachagua wagombea wa nafasi za udiwani, uwakilishi na ubunge katika jimbo la Nungwi linaendelea leo kwa utulivu na nidhamu ya hali ya juu.
Wajumbe kutoka maeneo mbalimbali ya jimbo la Nungwi wameendelea kujitokeza kwa wakati kushiriki mchakato huu muhimu wa kidemokrasia ndani ya chama cha mapinduzi.Hali ya uchaguzi ni shwari, maandalizi yamekamilika, na zoezi linafanyika kwa kufuata taratibu zote za chama.
Tunaendelea kuwapongeza wajumbe kwa mwitikio na ushiriki wao, pamoja na kuwahimiza kuendeleza amani na mshikamano katika hatua zote za uchaguzi huu.
#CCMImara
#UchaguziWaWajumbe2025
#NungwiYaKijani
