Alhamis 21-08-2025.
Katibu wa Baraza la Elimu Zanzibar ambaye pia ni Mrajisi wa Elimu Zanzibar, Farid Ali Mohammed, amewataka walimu wa Mkoa wa Kaskazini Unguja na Zanzibar kwa ujumla kuhakikisha wanajisajili na kupata leseni za kielektroniki ili kutekeleza majukumu yao kwa mujibu wa sheria.
Akizungumza jana katika ukumbi wa mikutano wa Ofisi ya Walimu Wilaya ya Kaskazini A, Mkwajuni, wakati wa ziara ya ugawaji wa leseni hizo, Katibu Farid alisema hatua hiyo ni muhimu kwa kuimarisha maendeleo ya walimu nchini.
Alifafanua kuwa leseni za kielektroniki zitasaidia serikali kufuatilia maadili ya walimu pamoja na kujua idadi kamili ya walimu nchini, jambo litakalosaidia katika kupanga na kuboresha miundombinu ya sekta ya elimu.
Farid aliongeza kuwa usajili wa walimu ni suala la kisheria ambapo kwa mujibu wa Sheria Namba 6 ya mwaka 1982, mwalimu atakayekiuka masharti hayo anaweza kutozwa faini ya shilingi 15,000 au kifungo kisichopungua miezi sita katika Chuo cha Mafunzo.
Kwa upande wake, Afisa Elimu Taaluma wa Mkoa huo, Mussa Said Salum, alisema leseni za kielektroniki ni hatua ya kimaendeleo, hasa katika dunia ya sasa iliyo ya kidigitali, na akahimiza walimu kuendelea kujisajili ili kuepuka changamoto zinazoweza kujitokeza katika utekelezaji wa majukumu yao.
Nao baadhi ya walimu walisema kuwa ujio wa leseni hizo ni hatua nzuri, lakini wakaomba Baraza la Elimu kurefusha muda wa usajili na muda zaidi wa kudumu leseni izo ili kuepuka usumbufu wa mara kwa mara na gharama zinazoweza kuathiri muda wao wa kufundisha wanafunzi.