Jumapili 24-08-2025.
Waandishi wa habari wametakiwa kutumia kalamu zao ipasavyo katika kuibua changamoto za rushwa, hasa zinazowakumba wanawake, kuelekea Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025 nchini.
Wito huo umetolewa leo na Yussuf Juma, kutoka Idara ya Elimu na Kinga ya Mamlaka ya Kupambana na Rushwa na Ujumu Uuchumi Zanzibar (ZAECA), katika mafunzo ya siku moja kwa waandishi wa habari kutoka Unguja yaliyofanyika ofisini za TAMWA–ZNZ, Tunguu, Wilaya ya Kati, Mkoa wa Kusini Unguja.
Amesema vyombo vya habari vina nafasi kubwa ya kuibua changamoto hizo na kuelimisha jamii, hasa katika kipindi hiki cha kuelekea uchaguzi mkuu. Aidha, amebainisha kuwa licha ya jitihada za kupiga vita rushwa kuendelea, bado wanawake wengi wanakumbwa na changamoto ya uoga wa kuripoti matukio ya rushwa, hali inayorudisha nyuma mapambano dhidi ya vitendo hivyo nchini.
“Rushwa ya aina yoyote ni kosa la jinai. Kupitia Sheria ya ZAECA iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2023, kifungu cha 98 na 99, mtu atakayetoa taarifa za rushwa analindwa kisheria kwa maslahi mapana ya taifa. Hii ni nafasi kubwa kwa wanawake kujitokeza na kutumia fursa za uongozi katika nyanja zote,” alisema Juma.
Kwa upande wao, wakufunzi wa mafunzo hayo Asha Abdi Makame, mwandishi mwandamizi Zanzibar, na Joel Ntile kutoka chombo cha habari The Chanzo, wamewataka waandishi kutumia vyanzo sahihi vya takwimu, pamoja na kuandaa makala na vipindi vya uchechemuzi vinavyohamasisha wanawake kushiriki uongozi. Walisema ni jukumu la wanahabari kubadili mtazamo mgando wa jamii dhidi ya nafasi ya mwanamke katika uongozi.
Washiriki wa mafunzo hayo waliishukuru TAMWA–ZNZ na wakufunzi kwa kuwaongezea maarifa na ujuzi, huku wakiahidi kuyatendea haki waliyoyapata kwa manufaa ya jamii, hususan katika kuwawezesha wanawake kufikia nafasi za uongozi nchini.
Akifunga mafunzo hayo kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa TAMWA–ZNZ, Safia Ngalape, alisema waandishi wanapaswa kujikita zaidi katika kuelimisha jamii juu ya sheria mbalimbali ili kumwezesha mwanamke kupaza sauti kwa maslahi mapana ya usawa wa kijinsia katika nyadhifa za uongozi nchini.