Na,Nishan khamis-Zanzibar.
Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi ya Zanzibar, Jaji George J. Kazi leo tarehe 31 Agosti, 2025 amekabidhi fomu ya uteuzi kwa mgombea wa Kiti cha Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kutoka Chama cha Kijamii (CCK), Isha Salim Hamad , Pamoja na Laila Rajab Khamis kutoka chama cha NCCR-Mageuzi, Laila Rajab Khamis h katika ofisi za Tume zilizopo Maisara, Wilaya ya Mjini Unguja.
ikiwa ni Wagombea 2 wanawake Pekee kati ya wagombea wa Vyama vyote kwa Upande wa Zanzibar kuwania nafasi hiyo katika uchaguzi Mwaka huu.
