Popular services

ZAIDI YA MILIONI 12 ZATUMIKA KUNUNULIA VYAKULA KWA AJILI YA KAMBI ZA SKULI ZA MATEMWE.

 MATEMWE.

Na,Nishan khamis kaskazini Unguja. 

Kamati ya uvuvi na kuhifadhi mzingira ya baharini matemwe imeto msaada wa vyakula vyenye thamani ya shilingi milioni kumi na mbili laki tatu na elfu hamsini kwa ajili ya kuwasaidia wanafunzi wanaokaa kambi kwa ajili ya kujianda na mitihani ya taifa pamoja na kuwahimiza wananchi wa kijiji hicho  katika utunzaji wa mazingira ili kuweka haiba nzuri kwa maslahi ya kijiji na taifa kwa ujumla.

Hayo ameyasema  katibu wa kamati ya uvuvi na mazingira kutoka shehia nne za matemwe   Ali Haji Kocha, wakati akizungumza katika kikao kilicho wakutanisha kamati ya uvuvi, walimu wakuu, masheha na wazazi  amesema baada ya kupata barua kutoka baadhi ya skuli wakaona ipo haja ya kutoa msaada huo ili uwasadie vijana hao katika katika kukuza elimu kwa wanafunzi.

Katibu amesema fedha izo zimetumika kununulia sukari, mchele,maharage,dagaa,mafuta chumvu i na vitu vingine vya upishi, aidha ametoa wito kwa wakaazi wa matemwe kuendelea kutunza mazingira ya baharini kwa maslahi ya yao vizazi vyao na taifa kwa ujumla.

Kwa upande wake sheha wa shehia ya Matemwe kaskazini Wadi Ali Wadi  amesema kuelekea kipindi hichi cha wanafunzi kujiandaa na mitihani ya taifa kiasi hicho kitawasaidia kwa kiasi kwa kujiandaa na mitihani yao hivyo  ametoa wito kwa wazazi, viongozi, wawekezaji na wadau mbali mbali kujitokeza katika kuwasaidia vijan hao katika kipindi hichi cha maandlizi ya mitihani yao ili kuweka mazingira bora ya kuwawezesha kufanya vizuri wanafunzi hao katika mitihani yao kwa kuwa na maandalizi bora. 

Naye Bakar jaha Mwadin mfanyakaizi wa Mnemba Island amesema anamshukuru na kumpongeza Rais Dkt Husein Ali Mwinyi kwa jitihada zake za maendeleo n kuweka safu nzuri ya usimamizi wa bahari kwa uhifadhi wa mazingira wenye tija ambapo amesema kiasi walicho toa kitasaidia kwa kiasi kwa kipindi hichi wanacho jiandaa na mitihani. 

Nao Mwalimu mkuu skuli ya sekondari Mtemwe Milimani Mariam Khamis Mwadin pamoja na mzazi Ulimwengu Mkadam Makame wametoa shukrani kwa msaada huo na kutoa wito kwa wazazi na walezi kushirikiana na walimu ili kutatua changamoto za utoro kwa wanafunzi kwani vijana wengi wanakata skuli kwa kujihusisha na shughuli za kitalii na uvuvi jambo ambalo linarejesha nyuma suala la maendeleo ya kielimu katika vijiji hivyo hivyo wametoa wito wameshauri kuandaliwa mikakati ya kutatau tatizo hilo.