BI LUCY MPEMBO, (MAMA AFRICA) AMECHUKUA FUMU YA UBUNGE JIMBO LA NUNGWI 2025
Nungwi, Unguja – Mwanamke shupavu na mwenye maono ya maendeleo, Bi Lucy Mpembo, ametangaza rasmi nia yake ya kugombea nafasi ya Ubunge wa Jimbo la Nungwi kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM) katika Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2025.Bi Mpembo ni mmoja wa wanawake wachache wanaojitokeza kwa ujasiri kugombea nafasi za juu za uongozi ndani ya CCM, akieleza kuwa ushiriki wa wanawake katika siasa ni msingi wa kuleta uwiano na usawa wa kijinsia katika uamuzi wa kitaifa.
