Popular services

BIG ACHUKUA FOMU YA UDIWANI WADI YA GAMBA.

 NYANGE KHERI ALI ACHUKUA FOMU YA UDIWANI WADI YA GAMBA, MKWAJUNI

Nishan Khamis. 

Kijana maarufu kwa jina la Big, Nyange Kheri Ali, amechukua rasmi fomu ya kuwania nafasi ya Udiwani katika Wadi ya Gamba, jimbo la Mkwajuni kupitia Chama Cha Mapinduzi (CCM).

Nyange ambaye ni miongoni mwa vijana wanaoheshimika na kupendwa katika eneo hilo, ameeleza dhamira yake ya kuwatumikia wananchi kwa moyo wa kujitolea, akiahidi kusimamia maendeleo ya jamii, hasa katika sekta za vijana, elimu na miundombinu.



Hatua yake imepokelewa kwa hisia tofauti na baadhi ya wakazi wa Gamba wakionyesha matumaini kuwa uongozi wake unaweza kuleta mageuzi chanya kwa maslahi ya wananchi wote.