*Na,Nishan khamis
wilaya ya kaskazini A Unguja* 📍
Waakazi wa shehia ya Kivunge jimbo la Kijini wilaya ya kaskazini A Unguja wameonesha kukasirika na tabaia ya baadhi ya watu kutumia eneo la hospital ya Kivunge katika kufanya vitendo vya utovu wa adabu ambavyo ni kinyume na utaratibu wa mila na desturi za mzanzibar.
Wananchi hao wameyasema hayo leo katika mkutano wa hadhara ulio andaliwa na jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya kaskazini A Unguja(NAPAC) ikiwa mwendelezo wa kusikiliza kero,changamoto na utoaji wa elimu ya sheria kwa wananchi wilya hiyo kwa misingi ya kutambua haki na wajibu wao katika kujenga msingi ya utatuzi wa changamoto kwa ujenzi wa maendeleo nchini.
Pia wemebainisha suala la ulevi kwa baaadhi ya vijana katika eneno hilo ni kero inayopelekea mmomonyoko wa maadili katika shehia hiyo na hutumia sehemu ya hospital na nje ya hospital kufanya matendo hayo ambayo ni kinyume na sheria na nchi na maadili ya mzanzibar.
Hivyo wamewashukuru NAPAC kwa ujio wao na kunufaika na elimu pamoja na kutoa changamoto zao huku wakisisitiza kuyafanyia kazi changamoto hizo kwa misingi ya kulinda upotevu wa nguvu ya taifa nchini kutokana na vijana kujihusisha na tabia ya vitendo viovu vinavyo pelekea mwenendo mbaya wa maisha yao.
Huweni Haji Juma sheha wa shehia ya Kivunge amekiri kuwepo kwa vitendo hivyo ambapo amesema suala la baadhi ya watu kufanya vitendo viovu eneo la hospital linatokana na sehemu ya upimaji wa watoto sehemu hiyo kukosa taa hali inayopelekea baahdi ya watu majira ya usiku kutumia eneo hilo kinyume na utaratibu mzuri mahala hapo.
Aidha amesema katika ufumbuzi wa tataizo hilo pamoja na ulevi kwa baaadhi ya vijana wameaanda mikakati madhubuti ya utatuzi wa changamoto hizo kwa misingi ya kuendelea kutunza amani na usalama katika shehia yake.
Amewataka wazazi kuacha muhali pindi doria itakapo anza katika shehia hiyo kwani mtoto au kijana atakaye kutwa na hatia sheria itafuata mkondo wake.
Halikadhalika amewashukuru NAPAC kwa ujio wao kwani jamii imefurahishwa na elimu waliyo ipata pamoja na kusikilizwa kero zao ikiwa ni mwendo mzuri wa kutatua changamoto za wanajamii nchini.
Nao wasaidizi wa sheria wakitoa ufafanuzi kwa baadhi ya changamoto wamesema suala la vitendo viovu watakaa na sheha na kamati za askari jamiii ili kutafuta njia mbadala za ufumbuzi wa tatizo hilo huku baadhi ya changamoto zingine wamezichukua na watazifikisha sehemu husika kwa misingi ya ufambuzi zaidi.