Popular services

*WAZIRI WA ARDHI AMEFANYA ZIARA YA KUTOA ELIMU YA ARDHI NA KUSIKILIZA CHANGAMOTO ZA MIGOGORO YA ARDHI WILAYA YA KASKAZINI A UNGUJA*


*Na,Nishan khamis*

*Wilaya ya kaskazini A Unguja*. 

Waziri wa Ardhi Maendeleo ya Makazi Mhe, Rahma Kassim Ali, leo amefanya ziara ya kutoa elimu ya masuala ya Ardhi pamoja na kusikiliza malalamiko na Changaomoto za wananchi wa shehia za Pwanimchangani, Kandwi na Matemwe Kusini zilizopo wilaya ya kaskazini A Unguja.

Akizungumza  na wananchia hao katika kiwanja cha mpira Pwanimchangani amesema zoezi hilo litakuwa endelevu  ili kupunguza changamoto hizo kwa kasi kubwa kwa misingi ya kuendelea kuimarisha amani na utulivu nchini. 

Mhe,Rahma amesema kupitia zoezi hilo kuna baadhi ya malalamiko yametatuliwa papo kwa papo ila baadhi ya changamoto  wamejichukua kwa misingi ya ufumbuzi wa upatikanaji wa haki zaidi.

Aidha amewashukuru na amewapaongeza wananchi kwa kuhudhuria mkutano huo, huku akiwataka waendelee kushirikiana na wizara pamoja na kuwa mabalozi wazuri wa kutoa elimu waliyo ipata kwa watu wengine ili kuongeza idadi kubwa ya elimu ya ardhi kwa jamiii. 

Mkuu wa wilaya ya kaskazini A Unguja Mhe, Othman Ali Maulid amemshukuru waziri na timu yake kwa kufika na kusikiliza malalamiko na changaomoto za ardhi ikiwa wilaya yake ni miongoni mwa wilaya zenye  changamoto kubwa za migogoro ya muda mrefu ikiwa migogoro hiyo ipo katika ngazi husika kwa ufumbuzi zaidi. 

Amemshahuri waziri na timu yake kushirikiana zaidi katika zoezi hilo liwe endelevu kwa misingi ya kuwaelimisha wananchi na kupunguza malalamiko na changaomoto za ardhi katika wilaya hiyo. 

Mh,Othman amewataka wananchi kufuata utaratibu wa ujenzi pindi wapo taka kujenga na kufuata taratibu za kuuza na kununua ardhi ili kuondoka malalamiko na changaomoto hizo katika wilaya hiyo.

Kwa upande wao wananchi wamesema kupitia ziara hiyo wamempngeza Mhe waziri kwa kuona umuhimu mkubwa wa kushuka chini na kuzifuata changamoto za wananchi wa chini ni jambo ambalo wamefurahishwa na kumpongeza kwa uwamuzi huo.

Hata hivyo wamesema kupitia ziara hiyo wameshukuru kupata elimu ,kukutana na viongozi mbali mbali na kueleza changamoto na baahdi yao kupatiwa ufumbuzi zaidi, huku wakisisitiza wizara na serikali kaa ujumla kufanyiwa mazi changamoto zao kwa misingi ya upatikanaji wa haki na kuendelea kutunza amani na utulivu nchini.