Popular services

*WAZAZI TIMIZENI WAJIBU WENU KWA WATOTO-NAPAC*


*Na,Nishan khamis-wilaya ya kaskazini A Unguja*

Wazazi wametakiwa kutimiza wajibu wao katika malezi ya watoto kwa kuwahimiza juu ya umuhimu wa elimu ya madrasa na skuli pamoja kuwalinda dhidi na vitendo vya udhalilishaji.

Hayo ameyasema mkurungezi wa wasaidizi wa sheria wilaya ya kaskazini A Unguja(NAPAC) Asia Fadhil Makame alipokuwa  akizungumza katika mkutano wa hadhara na wanakijiji wa  shehia ya Chaani Kikobweni kwa lengo la utoaji wa elimu ya sheria pamoja na kusikiliza changamoto na kero za kijiji hicho.

Mkurungezi wa taasisi ya wasaidizi sheria wilaya ya kaskazini A (NAPAC) Asia Fadhil Makame akizungumza na wanakijiji wa shehia ya Chaani Kikobweni.

Amesema uwepo wa changamoto za utoro wa skuli na madrasa unatokana  na ukosefu wa mashirikiano malezi ya pamoja ya wazazi hali inayopelekea  wanafunzi  kuwa watoro katika kijiji hicho jambo ambalo ni hatari kwaa watoto na vijana  vijana kujiingiza katika ulevi,wizi na utumiaji wa madawa ya kulevya ambapo ni athari kwa taifa la kesho.

Aidha Asia amesema NAPAC ipo kwa ajili ya msaada zaidi wa kisheria kwa misingi ya upatikanaji wa haki hivyo amewataka

 wanawake kuacha muhali juu watu wanao fanya vitendo vya udhalilishaji hata akiwa mumewe wahakikishe  wanaripoti kwa haraka vitendo hivyo katika vyombo husika kwa misingi ya kudhibiti na kutokomeza vitendo hivyo nchini. 

Ametoa wito kwa jamiii kuwatumia wasaidizi wa sheria pomoja na serikali kwa ujumla katika kujenga misingi ya upatikanaji wa haki kwa maendeleo ya kuimarisha amani na upendo nchini. 

Mkuu wa dawati la jinsia wanawake na watoto mkoa wa kaskazini Unguja Inspector Salum Khamis Machano amesema kesi nyingi za udhalilishaji zinazo ripotiwa katika dawati la jinsia katika mkoa huo kwa sasa ni vitendo vya utekelezaji wa watoto ambapo kupitia kifungu cha 7 sheria namba 6 mwaka 2011sheria ya mtoto Zanzibar imeeleza upatikanaji wa haki za mtoto kwa wazazi hata wakiwa wametengana ni wajibu kutimiziwa haki zao.

Inspector Salum amebainisha kuwa uwepo wa madawati ya jinsia si ya wanawake na watoto pekee bali ni watu wote hivyo amewataka wanaume kuripoti matukio ya udhalilishaji yoyote yanayo wakumba katika jamii zao.

Sheha wa shehia ya Kikobweni  Mcha Ali Mcha amekiri uwepo wa utoro wa watoto skulini na vyuoni katika shehia yake ,hivyo ameahidi kuandaa mikakati ya utatuzi wa changamoto hizo kwa misingi ya maendeleo ya watoto na taifa kwa ujumla. 

Kwa upande wao wananchi  wamesema suala ya utoro wa skuli na madrasa pamoja na vitendo vya wizi na uvutaji wa bangi na utumiaji wa madawa linatokana na muhali katika kijiji hicho.


Wamesema kupitia mkutano huo na elimu waliyoipata kwa kushirikiana na kamati za sheha wataandaa mikakati ya kutatuta changamoto hizo kwa misingi ya malezi bora ya watoto na pamoja na kuondoa vitendo vya kihalifu katika kijiji chao.