Popular services

UWT WAKEMEA VITENDO VYA UDHALILISHAJI NA UKATILI WA KIJINSIA NCHINI

 Katibu wa umoja wa wanawake Tanzania(UWT) wilaya ya kaskazini A Unguja Mtenge Makame Faki amewataka wanawake wa nungwi na wilaya kwa ujumla  kuwa mstari wa mbele kuendelea kupiga vita vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia ulipo katika wilaya hiyo.


Katibu Mtenge alisema hayo leo katika kiwanja cha mpira Hamburu Nungwi katika kilele cha maadhimisho ya siku ya umoja wa wanawake Tanzania yaliyo anadaliwa na UWT wilaya hiyo.


Alisema wanawake wanatakiwa kuendelea kushijiishana katika kuendelea kukemea vitendo vya udhalilishaji  hasa kwa watoto ambao wao ndio wahanga wakubwa wanao kumbana na vitendo hivyo.


Alisema UWT kupitia maadhimisho hayo yaliyo ambatana na ziara ya kukagua miradi mbali mbali ya maendeleo alisema  wanaendelea kukemea  vikali vitendo hivyo vinavyo endelea kuwepo katika jamiii na kurudisha nyuma malengo ya watoto.


Halikadhalika amesema uwepo wa miradi masoko katika wilaya hiyo ni usimamizi mzuri wa Dkt Husein Ali Mwinyi katika utekelezaji wa ilani CCM hivyo amewahamssisha wanawake kuchangamkia fursa za masoko hayo katika kujiendeleza katika ujasirimali na kujiinua kiuchumi. 


Mwenyekiti wa CCM wilaya hiyo Ali Makame Khamis (Dilunga) amesisitiza wanawake na vijana kuchangamkia fursa za masoko yaliyopo katika wilaya hiyo kwani suala kujiimarisha kimaisha si lazima upate ajira ya serikali kupitia biashara na ujasirimali ni njia moja wapo nzuri ya kujikwamua kiuchumi kwa misingi ya maendeleo ya mtu mmoja mmoja na taifa kwa ujumla.



Aidha amewasisitiza vijana kushiriki ipasavyo katika ujenzi wa maendeleo yanayo endelea katika wilaya hiyo ikiwa wao ndio nguvu kubwa ya taifa katika maendeleo na kuwa mstari wa mbele zaidi pamoja na kukemea vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia katika wilaya,mkoa na taifa kwa ujumla.


Akizungumza katika maadhimisho hayo kwa niaba ya mkuu wa polisi wilaya hiyo mkuu wa kituo cha Polisi Nungwi,Asp Zauda Juma alisema suala la kukabiliana na vitendo vya udhalilishaji ni lazima jamanii ushirikiane ipasavyo na watoto wapewe elimu ya kujikinga na vitendo hivyo mapema ila viwasaidie katika mazingira yao ya kila siku.


Amewataka vijana kuwa mstari wa mbele kukemia vitendo hivyo uku wazazi na  walezi kuwa karibu na kusikiliza changamoto za watoto wao kwa misingi ya kuwaepusha kuingia katika vitendo hivyo harakati kutoka halo iliyopo inavyo endelea kuripotiwa katika vituo vya polisi na mamlaka na vyombo vya habari nchini. 


Amesisitiza endapo jamii ikashirikiana na kuacha masaula ya muhali na vyombo vya sheria vikafuta mkondo wake ipasavyo basi vitendo hivyo vitatoweka inchini.


Mjumbe wa kamati tekelezaji UWT bi Rahma Abdalla Maisara alisema kupitia ziara hiyo wameridhishwa kwa aslimia zote utekelezaji wa ilani ya chama cha mapinduzi,hivyo wataendelea kuunga mkono juhudi za rais Dkt Husein Ali Mwinyi pamoja na Dkt Samia Suluhu Hassan.