Popular services

*WAZAZI HOFU ZATAWALA UWEPO WA SHIMO KUBWA ENEO LA SKULI*


*Na,Nishan khamis-wilaya ya kaskazini A Unguja*

Wazazi na walezi shehia ya Chaani Kikobweni wilaya ya kaskazini A Unguja wamejawa na hofu ya usalama mdogo kwa watoto wao wa skuli ya nasari kikobweni kutokana na shimo kubwa lililopo karibu na skuli.

Hayao yamejiri leo katika mkutano wa hadhara uliondaliwa na jumuiya ya wasaidizi wa sheria wilaya ya kaskazini A Unguja (NAPAC) mkutano huo uliofanyika katika skuli ya Chaani Kikobweni wenye lengo la kutoa elimu ya sheria pamoja na kusikiliza kero na Changaomoto za wanakijiji wa Kikobweni.

Wanakijiji hao wakizungumza kero zao katika mkutano huo wamesema uwepo wa shimo kubwa la kisima kilicho wazi eneo la skuli ya nasari ya Kikobweni inapelekea wazazi wengi kuwa na hofu kwa watoto wao kutoka na usalama mdogo kulingana na hatari ya uwepo wa shimo la kisima.

Hivyo wamewaomba NAPAC pamoja na viongozi wa jimbo hilo na serikali kwa ujumla kutafuta njia ya kupata ufumbuzi wa shimo hilo pamoja na kutengeneza kisima chao cha maji kwa misingi ya kuimarisha maendeleo ya shehia hiyo zaidi.

Maafisa kutoka NAPAC baadhi yao kutokana na ukubwa na tatizo hilo wamaesema watahakikisha wanalifanyia kazi suala hilo hataka kwa misingi ya kuweka amani na utulivu wa wazazi juu ya watoto wao wakiwa skuli.

Aidha wamewasisitza wananchi kuendelea kutumia katika ya nchi ya kutoa maoni na kuwa na uhuru wa kueleza changamoto na kero mbali mbali kwa misingi ya utatuzi na ufumbuzi wa matatizo yao zaidi.