Popular services

*KAMISHENI YA UTALII IMEFANYA DORIA YA VIBALI VYA WATEMBEZA WATALII*


*Na,Nishan khamis wilaya ya kaskazini A Unguja*


Kamishina ya utalii Zanzbar leo tarehe 19/10/2024 imeendelea na doria ya ukaguzi wa vibali vya watembezaji na wabebaji wa watalii nchini. 


Akizungumza katika zoezi hilo huko kibwengo Fukuchani wilaya ya kaskazini A Unguja afisa msaidizi mratibu kitengo cha utalii na diplomasia kamisheni ya utalii Zanzibar Talib Shaban Rajab, amesema lengo la  zoezi hilo ni kushajiisha ukataji wa vibali vya kuwatembeza  watalii  pamoja na ukataji wa stika za gari za privete here na zile za kampuni kwa lengo la kuimarisha usalama wa watilii nchini. 

Amesema bado kuna changamoto kwa baadhi ya vijana wamejiwekeza katika masuala ya utalii pasi na kuwa na leseni ya shuguli hizo ikiwa ni kinyume na taratibu za nchi. 


Amebainisha kuwa katika ziara hiyo wamebaini uwepo wa gari za kampuni zinazo chukua watalii zisizo na leseni pamoja na ukwepaji wa ukataji vaibali vya kuwabebea wageni japo ambalo limepelekea kukosa pato la taifa na kutokana na hilo  wamechukua hatua za faini za papo kwa papo kwa misingi ya kuimarisha ulipaji kodi kwa maendeleo ya nchi. 


Aidha amewahimiza  wanajihusisha na shuguli za kitalii kukata leseni zao kwa utaratibu ili kuondoa usumbufu wa kusimamishwa mara kwa mara barabarani jambo ambalo ni kero kwa wageni.

Pia amewasisitiza kujiongeza kielimu zaidi ili kufanya kazi kwa ufanisi na kuzingatia na kufuata sheria na taratibu za utalii kwa usalama wa watalii na maendeleo endelevu ya utalii nchini kwa misingi ya kuongeza pato la taifa.


Idi Ali na Salim khamis ni miongoni wanao jishughurisha na utalii wamesema ukosefu wa ofisi maalum ya ukataji vibali,ulipaji wa kodi kwa wingi pamoja kusimamishwa mara kwa mara barabarana ni kero kwao inayopelekea watalii wengi kuuliza juu ya usumbufu huo njiani. 


Wameimba kamisheni na serikali kwa ujumla kupunguziwa kodi,wajengewe ofisi maalum za ukataji vibali ili kupunguza tatizo la kusimamishwa mara kwa mara njiani.