*MBUNGE JUMA USONGE WA CHAANI AZINDUA NDONDO CUP 2024,AHAHIDI KUENDELEA KUSIMAMIA VIPAJI KATIKA JIMBO LAKE*
*Na, Nishan Khamis -Jimbo la Chaani*
Mbunge wa Jimbo la Chaani Mhe. *Juma Usonge Hamad* leo amefungua mashindano ya Mpira ya Ndondo cup 2024 yalioandaliwa na wadau wa mpira kutoka Banda Maji, katika mashindano hayo ambayo yatakayorindima kwa mwezi mmoja timu zaidi ya 12 kutoka Jimbo la Chaani na Mahonda zitashiriki,
Mhe. Usonge amewaahidi vijana hao kuendelea kushirikiana nao kama ilivyo desturi yake kuwasapoti vijana hususan katika michezo na ameahidi mashindano ya mara hii ni kutegemea zawadi nzuri kuliko miaka mengine iliyopita pomoja na kuendelea kuimarisha michezo na kuibua vipaji kwa vijana jimbo lake.
Katika ufunguzi huo uliochezwa katika kiwanja cha Banda Maji, timu ya Kandwi heroes ilishinda mabao 2 na Banda Maji Academy bao 1.
