Na, Nishan khamis-Jimbo la Chaani
Mbunge wa jimbo la Chaani pia ni mjumbe wa Halmashauri kuu ya Chama Cha Mapinduzi mkoa wa kaskazini Unguja Mhe,Juma Usonge Hamad leo amekabidhi vifaa vya ujenzi wa maskani ya wanachama wa CCM Chaani Masingini jimbo la Chaani wilaya ya kaskazini A Unguja.
Usonge amekabidhi Bati za kisasa,misumari,miti,Gysam,ties,mchanga na kokoto kwa misingi ya kuendelea kuimarisha maskani katika Jimbo hilo.
Usonge amesema hiyo ni maskani ya tano katika jimbo hilo na ataendelea kuziimarisha maskani mbali mbali katika jimbo hilo kwani maskani hizo ni chimbuko la Mapinduzi yetu ya Zanzibar lakini pia Mhe. Usonge amesema sio watu wote wanaweza kuingia Matawi na badala yake wanaishia katika maskani hiyo.
Amewasisitiza kuendelea kufanya kazi kwa pamoja kwa ushirikiano mkubwa katika kuendeleza kukiimarisha chama cha mapinduzi katika ngazi zote.
Kwa upande wao watumiaji wa maskani hiyo wamesema wamefurahishwa na utekelezaji wa ahadi ya mbunge katika ujenzi wa maskani yao kwani walikuwa katika kibanda lakini sasa mpaka ikikamilika itakuwa maskani ya kisasa zaidi.
Aidha wamesema bado wataendelea kuunga mkono juhudi zake katika jimbo hilo pamoja na juhudi za marais wote nchini kwa maendeleo wanayo fanya nchini.

