UGUMU WA MAISHA CHANJO CHA VIJANA KUINGIA KWENYE MAKUNDI MAOVU.
Na,Nishan khamis-kaskazin unguja
Waakazi wa Kinduni na Mgambo wilaya ya kaskazin "B" Unguja wamesema miongoni mwa sababu zinazo sababisha vijana wengi kuingia katika makundi maovu hivi sasa ni kutokana na ungumu wa maisha nchini.
Wakaazi hao wameyasema hayo hapo jana katika mkutano wa hadhara uliofanyika katika maduka ya wajasiriamali kinduni ikiwa ni muendelezo wa ziara za mkuu wa mkoa kaskazin unguja Mheshimiwa Ayoub Mohommed Mahmoud za kusikiliza kero na Changaomoto za waakazi wa shehia 75 kwenye mkoa huo na kutafuta ufumbuzi wa kero hizo.
Wamesema baadhi ya vijana wamekuwa wakikata tamaa za maisha na kujiingiza katika utumiaji na uuzaji wa madawa ya kulevya, uvutaji bangi na kujiunga na vikundi viovu, wananchi hao wamemuomba mkuu wa mkoa na serikali kwa ujumla kulingalia suala hilo na kulipatia ufumbuzi kwa maendeleo ya taifa.
Akilitolea ufafanuzi suala hilo mkuu wa mkoa amesema tatizo la ugumu wa maisha janga la dunia hivi sasa kutokana na upandaji wa dola na kushuka thamani ya fedha ya Tanzania, uzalishaji mdogo wa ndani kwenye mazao ongezeko la bei za makontena na vita vya Urus na Ukraine ni sababu kuu za ungumu wa maisha Zanzibar na Duniani .
RC Ayoub amesema serikali imeandaa mipango madhubuti ya kilimo cha kisasa zaidi na umwagiliaji na amewasajiisha wanajamii kuunga mkoa juhudi za serikali katika uzalisha na wao kutumia kilimo cha kisasa ili kuongeza kiwango kikubwa cha uzalishaji wa chakula Nchini.
