Popular services

 Mwandishi, Nishan khamis, Zanzibar. 

Diwani wa Kuteuliwa Wilaya ya Kaskazini ‘A’, Chembe Khamis Sheha, amejumuika na Sheha wa Shehia ya Potoa pamoja na wananchi katika zoezi la kufanya usafi lililofanyika katika maeneo mbalimbali ya shehia hiyo, ikiwa ni sehemu ya kuimarisha usafi wa mazingira na afya za jamii.

Akizungumza wakati wa zoezi hilo, Diwani Chembe Khamis Sheha amesisitiza umuhimu wa wananchi kudumisha usafi wa mazingira ili kulinda afya zao na kuzuia magonjwa.

Amesema serikali inaendelea kuhamasisha ushirikiano kati ya viongozi na wananchi katika kuhakikisha mazingira yanakuwa safi na salama.

Naye Sheha wa Shehia ya Potoa, Sheha Khamis Juma, amepongeza ushirikiano kati ya uongozi na wananchi katika shughuli za usafi, akisema umeongeza mshikamano na hamasa ya kulinda mazingira.

Wananchi wa Shehia ya Potoa wameeleza kufurahishwa na ushiriki wa viongozi wao, wakiahidi kuendelea kushiriki kikamilifu katika shughuli za usafi kwa maendeleo ya jamii yao.