Mwandishi:Nishan Khamis, Zanzibar.
Diwani wa Wadi ya Kijini, Faki Zubeir Haji (BERA), leo amefungua rasmi mashindano ya mpira wa miguu ya Ndondo Cup yatakayoshirikisha jumla ya timu 14 kutoka Wadi za Kijini na Kidombo, huku akisisitiza umuhimu wa michezo katika kukuza vipaji vya vijana na kuimarisha mshikamano wa jamii.
Akizungumza katika ufunguzi wa mashindano hayo uliofanyika katika Kiwanja cha Nyundo FC, BERA amesema michezo ni nyenzo muhimu ya kuwaunganisha vijana, kuimarisha afya zao na kuwapa fursa ya kuonesha vipaji ambavyo vinaweza kuwafungulia milango ya maendeleo katika siku zijazo.
Amesema Serikali ya Zanzibar chini ya uongozi wa Dkt. Hussein Ali Mwinyi imeendelea kuweka mazingira mazuri ya maendeleo ya michezo kupitia ujenzi na uboreshaji wa viwanja vya kisasa katika ngazi mbalimbali, jambo linalodhihirisha dhamira ya serikali ya kuendeleza sekta hiyo.
Diwani huyo aliwataka vijana kushiriki mashindano hayo kwa nidhamu, kuzingatia sheria za mchezo na kuendelea kudumisha amani, umoja na mshikamano ili michezo iwe chachu ya maendeleo badala ya migogoro.
Kwa upande wao, washiriki wa mashindano hayo wamempongeza Diwani BERA kwa kuanzisha mashindano hayo wakisema yatawasaidia vijana kutumia muda wao katika shughuli zenye manufaa, kukuza vipaji vyao na kujiepusha na vitendo viovu ikiwemo matumizi ya dawa za kulevya, uhalifu na makundi yasiyo na tija kwa maendeleo ya jamii.
Mashindano hayo yameanza leo kwa mchezo wa ufunguzi uliowakutanisha Mbuyu Popo FC na Kibuyuni FC katika Kiwanja cha Nyundo FC. Waandaaji wamesema mshindi wa mashindano hayo atajinyakulia mbuzi pamoja na vifaa vya michezo mara baada ya kumalizika kwa ligi hiyo.