Popular services

 Mwandishi, Nishan khamis, Zanzibar . 

Diwani wa Kuteuliwa Wilaya ya Kaskazini A, Mheshimiwa Jabu Hamdu Makame, leo ameadhimisha siku yake ya kuzaliwa kwa kufanya ziara maalum ya kijamii ya kumtembelea na kumfariji mama aliyejifungua watoto pacha watatu katika Jimbo la Mkwajuni.


Ziara hiyo imefanyika ikiwa ni sehemu ya kuonesha upendo, mshikamano na kuthamini jamii, hususan katika kipindi hiki kuelekea Wiki ya Mtoto wa Afrika, ambapo jamii hukumbushwa wajibu wa kulinda, kulea na kuwahudumia watoto kwa upendo na usawa.

kwa upande wake Katibu wa (UWT) Wilaya hiyo Mtenge Makame Faki,  amempongeza diwani huyo kwa hatua yake ya kutumia siku yake ya kuzaliwa kufanya jambo la kijamii lenye kugusa maisha ya watu.

Katibu Mtenge amesema kitendo hicho ni mfano wa uongozi unaojali wananchi na kuimarisha mshikamano katika jamii, hususan katika kipindi ambacho taifa linaelekea kuadhimisha Wiki ya Mtoto wa Afrika.

Amesema watoto ni nguzo muhimu ya taifa la kesho, hivyo jamii inapaswa kuwa karibu na familia zinazopata changamoto au baraka kubwa kama ya kupata watoto wengi kwa wakati mmoja, ili kuwapa faraja na msaada wa kimaadili na kijamii.

Naye mama wa watoto hao, Suhaila Juma Makame, ametoa shukrani kwa viongozi hao kwa kumtembelea na kumfariji, akisema ujio wao umempa nguvu na faraja kubwa katika kipindi hiki cha malezi ya watoto wake.
Amesema kitendo hicho kimeonesha wazi kuwa viongozi wako karibu na wananchi na wanajali changamoto na furaha za jamii