Popular services

USONGE AHIDI KUSHIRIKIANA NA VIJANA KATIKA MICHEZO JIMBO LA CHAANI

Na,Nishan khamis. 

P/Mchangani Jimbo la Chaani 

Mbunge wa jimbo la Chaani Juma Hamad Usonge amesema ataendelea kuanzisha michezo mbali mbali katika jimbo lake na kusimamia vipaji hivyo kwa misingi ya kuwainua vijana katika michezo na kuweza kujiajiri na kuajiriwa kupitia michezo mbali mbali.

Kauli hiyo Usonge ameisema hapo  jana katika kijiji cha Pwanimchangani wilaya ya kaskazini A katika bonanza la michezo mbali mabli lenye lengo la  shamra shamra za kueleka maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar pamoja na kumpongeza Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Husein Ali Mwinyi kwa jitahada za kuimarisha sekta ya michezo nchini. 

Amesema kutokana na jitihada kubwa za rais anazo fanya katika sekta mbali mbali kupitia sekta ya michezo rais amendelea kuimarisha miundoni imara ya viwanja na michezo mbali mbali jambo ambalo ni fursa kwa viongozi wengine kuendelea kumuunga mkono rasi katika kuwasaidia vijana katika michezo kwa misingi ya maendeleo ya vijana na taifa kwa ujumla.

Masoud Abullah ni mshindi wa kwanza  katika mashindano ya baiskel  kilometa 21 katika bonanza hilo amesema amemshukuru mbunge kwa kuanzisha bonanza hilo jambo ambalo limepeleka watu wengi khina kipaji chake katika kewendesha baskel kwani michezo ni ajira,inaimarisha afya ,kujenga udugu na kujenga ushirikiano katika jamii  na watu mbali mbali ambapo amesema siri ya mafanikio yake katika shindano hilo ni jitihada za mazoezi ya mara kwa mara anayofanya.

Naye Bahat Abdalla Hassan ni miongoni mwa wachezaji wa nage kutoka timu ya Pwanimchangani amesema amefurahishwa na michezo mbali mbali iliyojiri katika bonanza hilo hivyo amemuomba mbunge kuendelea kufanya hivyo kwa misingi ya kuinua vipaji kaa vijana jimboni kwake ila kuweza kujiajiri na kuwajiriwa kupitia michezo. 


Michezo mbali mbali iliyofanyika katika bonanza hilo ikiwemo riadha, mbio za baskeli kilometa 21,kufukuza upepo, nage,karata,bao,draft, maigizo na Sanaa mbali mbali zilichukua nafasi katika bonanza hilo lililo andaliwa na mbunge wa jimbo hilo.