Popular services

RC, MATTAR AANZA NA WATUMISHI WA MKOA

Na,Nishan khamis. 

Mkoa wa kaskazini Unguja. 

Mkuu wa mkoa wa kaskazini Unguja Mhe Mattar Zahor Masoud amewaomba watumishi wa ofisi ya mkuu wa mkoa huo  wote kwa ujumla kumpa mashirikiano katika pamoja na kuleta ufanisi wa majukumu yao ya utendaji katika kuimarisha ya ofisi na mkoa kwa ujumla. 

Mhe, Mattar ameyaemea hayo leo uko ofisini kwako mkokotoni wilaya ya kaskazini A wakati wa utambulisho wake na watumishi wa ofiisi hiyo kwa misingi ukaribisho ofisini hapo kwa lengo ya kuimarisha ushirikiano na mshikanamo katika utendaji wa majukumu yao.

Amesema suala la ushirikiano lina umuhimu mkubwa na uwepo wa ofisi hiyo ambayo inamajukumu makubwa katika kuratibu masuala mbali mbali kila mtumishi anahaki ya kuwajibika na kufanya kazi kwa mujibu wa mujukumu yake katika kuleta ufanisi zaidi kwa maendeleo ya ofisi, mkoa na taifa kwa ujumla. 

Amefahamisha kuwa ofisi hiyo siyo ya mtu bali ni taasisi ambayo inahitaji mashirikiano, upendo,ufanisi na uwajibikaji katika kuwatumikia wananchi kwa pamoja kwa  misingi ya utatuzi wa changamoto ,kuratibu mambo mbali mbali na kuendelea kudumisha amani na utulivu ndani ya mkoa na taifa kwa ujumla.

Amewataka watumishi wote kuzingatia suala la nidhamu katika mahudhurio ya kazini, kuja na kuondoka kama utaratibu ulipangwa kisheria pamoja na kufuata kanuni na sera ya ajira kwa watumishi katika uwajibikaji wa majukumu yao huku akisisitiza upokeaji na usikikizaji mzuri kwa wananchi wote watakao fika ofisini wapatiwe huduma nzuri ili kujenga taswira nzuri katika kuwajibikia wananchi.

Aidha amewahakikishia kushughulikia matatizo ya ofisi pamoja na kuwataka kutunza rasilimali zote na kuepukana na vitendo vya marumbano na migogoro ambayo inaweza kurejesha nyuma malengo ya kimaendeleo katika ofisi na mkoa kwa ujumla.

Kwa upande kaimu katibu tawala  pia ni afisa mkuu utumishi mkoa huo Miza Hassan Mussa akizungumza kwa nianba ya watendaji wenzake amemmkaribisha Mhe Mattar huku akimuahidi kushirikiana naye katika nyanza zote katika kuleta ufanisi zaidi wa utekelezaji wa majukumu 

Aidha amewataka wananchi mkoa wa kaskazini Unguja kumpokea mkuu wa mkoa na kuonesha ushirikiano naye katika utatuzi wa changamoto na kuimarisha maendeleo na kudumisha amani na upendo katika mkoa na taifa kwa ujumla.