Popular services

MBUNGE USONGE:TUNA KILA SABABU YA KUYAENZI MAPINDUZI YA MWAKA 1964.


Na,Nishan khamis. 

Jimbo la Chaani. 

Mbunge wa jimbo la Chaani Juma Hamad Usonge amesema  wananchi wa jimbo la Chaani na Zanzibar kwa ujumla wanakila sababu ya kuyaenzi na kuyatunza mapinduzi ya Januari 1964 kutokana na kujitoa kwa wazee wetu kuyapambani Mapinduzi na kuondoa udhalimu wa ukoloni  jambo ambalo limeleta  matunda makuwa nchini. 

Usonge ameyasema hayi hapo  jana katika kijiji cha Pwanimchangani kilichopo jimbo la Chaani wilaya ya kaskazini A alipokuwa akizungumza na wananchi  na  wageni mbali mbali waliohudhuria  katika bonanza la michezo mbali mbali ikiwa ni  shamra shamra za kuazimisha miaka 61 ya Mapinduzi pamoja na kumpongeza Rais wa Zanzibar na mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt Husein Ali Mwinyi  kutokana na utekelezaji wake wa ilani ya chama cha mapinduzi kwa muda mfupi katika madaraka yake.

Amesema  kutokana na umuhimu mkubwa wa mapinduzi ameamua kuandaa bonanza hilo ili kuonesha vijana thamani ya kuyaenzi Mapinduzi pamoja na kumpongeza rais Dkt Husein Ali Mwinyi kutokana na jitahada zake za kuimarisha miundoni katika nyanza zote inchini kwa  kipindi kifupi cha mabadaraka yake ni jambo la kumuunga mkono kwa asilimia zote na kumpongeza kwa utekelezaji mzuri wa ilani ya CCM mwaka 2020 -2025  kutokana na makubwa aliyotekeleza kwa kuweka miundoni imara ya afya, barabara,michezo, elimu na kuimarisha mishahara kwa watumishi na penshen jamii kwa wazee ni mambo muhimu ambayo ameyafanya na anapaswa kupongezwa na kumuunga mkono 2025 katika uchanguzi mkuu nchini ili kuendelea kuiongoza nchi.

Pia amempongeza Dkt Samia Suluhu Hassan rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa jitihada kubwa anazo zifanya za kimaendeleo katika kuwainua wananchi kiuchumi na kuendelea kuimarisha miundoni nchini hivyo amewataka wananchi kuunga mkono juhudi za viongozi pamoja na kujitokeza kwa wingi katika uandikishaji wa awamu ya pili  katika daftari la wapiga kura  linalo tarajiwa kuanza mwezi febuari 2025.

Usonge amewashukuru viongozi na wananchi waliohudhuria katika bonanza hilo amewataka kuendelea kushirikiana ili kuleta maendeleo ya jimbo hilo huku akiwahidi kuendelea kuimarisha michezo kwa kuibua vipaji  ili vijana waweze kujiajiri na kuajiriwa kwa maendeleo ya jimbo na taifa kwa ujumla.

Nao baadhi ya washiriki wa michezo katika bonanza wamesema wamefurahishwa na mbunge kwa kuandaa bonanza hilo kwa kuwajumisha rika zote na michezo ya aina mbali mbali kwani michezo inaumuhimu mkubwa katika maisha ya binadamu hivyo wamefarjika sana na tukio hilo katika jimbo lao na wamemuhidi mbunge kuendelea kushirikiana naye katika nyanza zote kutokana na ushiriki wake kwa jamiii ni jambo la muhimu kwa kujenga misingi ya maendeleo katika jimbo lao.

Bonanza hilo limejuimisha michezo ya aina mbali mabli akiwemo mbio za riadha,mbio za baiskeli,mchezo wa nage, karata,bao,drafti,kufukuza upepo,kukimbiza kuku,unywaji wa soda na vikundi mbali mbali vya sanaa na maigizo vilishiriki ipasavyo ambapo washindi na washiriki mbali mbali walipewa zawadi ikiwa lengo kuu la  bonanza ni  shamra shamra za maadhimisho ya miaka 61 ya mapinduzi ya Zanzibar na kumpongeza rais Dkt Husein Ali Mwinyi kwa kutekeleza ipasavyo ilani ya CCM ikiwaa bonanza hilo limeandaliwa na mbunge wa jimbo la Chaani Mhe Juma Usonge.