Na,Khamis Nishan.
Mkwajuni W/Kaskazini A Unguja.
Jumuiya ya vijana na elimu wilaya ya kaskazini A Unguja (JUVIEKA) kwa kushirikiana na taasisi ya Actionaid Zanzibar na Global Platform Tanzania wameweza kuwafikia vijana 600 kutoka mkoa wa kaskazini Unguja kwa lengo la kuwapa elimu ya uwelewa wa sera ya maendeleo ya vijana mwaka 2023 Zanzibar kwa misingi ya ufahamu wa vijana mikakati ya serikali katika kuwainua kiuchumi, kijamii na kisiasa nchini.
Hayo ameyasema mwenyekiti wa Juvieka Mbarouk Maalum Mohammed leo katika ukumbi wa mikutano kituo cha walimu mkwajuni wilaya ya kaskazini A Unguja akizungumza na maafisa wa vijana wilaya zote za kaskazini Unguja, vijana na wadau mbali mbali wakati akifanya tathimini ya uwelewa wa vijana juu ya sera ya maendeleo ya vijana Zanzibar mwaka 2023.
Mbarouk amesema kutokana na umuhimu mkubwa wa uwepo wa vijana nchini wameona ni jambo la msingi kuwapa elimu vijana kuhusu sera maendeleo ya vijana mwaka 2023 ili watambue dira,dhamira na lengo kuu la sera kwa vijana ili kuwajenga kuwa wazalendo na kuwainua kiuchumi,kijamii na kisiasa kwa misingi ya maendeleo ya vijana na taifa kwa ujumla.
Amebainisha kuwa bado kuna changamoto kubwa kwa vijana kuifahamu sera hiyo hivyo jitahada za serikali na taasisi binasfi zinaitajika kuwaelimisha vijana juu sera kutambua azma ya serikali yao katika kuwainua kiuchumi,kijamii kisisasa na utatuzi wa changamoto mbali mbali zinazo wakabili vijana nchini.
Pia amewahasisha vijana kujiunga na mabaraza ya vijana kwani yanaumuhimu wake katika upatikanaji wa fursa mbali mbali za kimaendeleo na ameishauri idara ya maendeleo ya vijana Zanzibar kuangalia vizuri uimarishawaji wa baraza ya vijana ngazi zote nchini kwa misingi ya kuimarishwa kuichumi na kujitegemea kwa misingi ya maendeleo ya vijana.
Halikadhalika ameeleza kuwa juvieka inafanya kazi katika maeneo matatu ambayo ni kuhimiza uwajibikaji, kifanya ushawishi wa sera za maendeleo pamoja na kuwasaidia kimaendeleo vijana ,wanawake, watoto na watu wenye ulemavu, hivyo amesisitiza kuwa wataendele kuwajibika kwa misingi ya maendeleo ya vijana ya mkoa huo na ameomba ushirikiano kwa serikali,jamii na wadau mbali mbali katika ujenzi wa maendeleo ya vijana nchini.
Fat-hiya Rashid Haji kutoka shehia ya Gamba ni miongoni mwa vijana waliofikiwa na elimu ya utambuzi wa sera amesema kupitia elimu ya sera ya maendeleo ya vijana 2023 aliyoipata imemnufanisha kwa kiaisi kikubwa kujua wajibu wake kijana nchini katika kwajibika katika kupiga vita vitendo vya udhalilishaji, kupinga vita vitendo vya rushwa pamoja na kutunza amani na utulivu uliopo nchini.
Naye Rajab Muhidin Atai mwenyekiti wa baraza la vijana Shehia ya Mahonda ameiopongeza serikali kwa maono yao kufanikisha sera ya maendeleo ya vijana mwaka 2023 hivyo ameiomba serikali kuendelea kuipa nguvu na kushirikiana na Juvieka na taasisi mbalimbali katika kuwainua vijana kimaendeleo katika nyanza zote nchini.
Akitoa ushuhuda wa kunufaika na elimu hiyo Salma Nyange Abdalla mkaazi wa Gamba amesema baada ya kupata elimu iyo amekuwa balozi mzuri kwa vijana wenzake katika kuwaelimisha ambapo amefanikiwa kumuelimisha kijana mwenzake aliyekuwa anataka kuingia katika matumizi ya madawa ya kulevya hivyo kupia wajibu wa vijana katika sera hiyo alimuelimisha kijana huyo na kumsadia kumuepusha na matumizi ya madawa ya kulevya baada ya kumpatia elimu aliyo pata.
Pia baadhi ya vijana wamesema licha ya uwepo wa sera hiyo bado sera inachagamoto kwa baadhi ya maeneo kwani sera haija eleza ujumishi wa kimichezo kwa watu wenye uleamavu, sera haija fafanua kujiendesha kwa mabaraza ya vijana nchini hivyo wameimba juvieka kuendelea kuishauri serikali katika kuangalia changamoto zilizopo kwenye sera kwa kujenga maendeleo ya vijana nchini kwa hali zote.
Elimu ilianza kutolewa mwezi Agosti 2024 hadi mwezi Disemba kwa kutumia njia ya kufanya kongamano la vijana mkoa wa kaskazini Unguja,mafunzo kwa baadhi ya vijana na kuzifikia shehia kwa sheia mkoa huo na kufika idadi ya vijana mia sita waliopatiwa elimu hiyo.


