Na,Nishan khamis.
Wilaya ya Kaskazini A Unguja.
Mwenyekiti wa Globify Charity Tanzania Gama Mwanga ameishauri jamii kuitumia vizuri mitandao ya kijamii katika kuwasaidia na kutatua changamoto mbali mbali kwa watu wenye mahitaji maalumu nchini
Mwenyekiti Gama ameyaema hayo leo alipotembelea kituo cha kulelea watoto yatima cha Salim Turky Foundation kilichopo kijiji cha kandwi wilaya ya kaskazini A Unguja ambapo amesema lengo la kufika kituoni hapo na ujumbe wake aliongozana nao kutoka Tanzania bara ni jkuwatembelea watoto yatima,kuwafariji pamoja na kuwapa misaada mbali mbali kulingana na changamoto zilzokuwa zinawaalabili kituoni hapo.
Amesema misaada yote aliyofikisha kituoni hapo imetokana na kuchangiwa na wadau wa Globify Charity Tanzania ikiwa ni malengo yao kuendelea Kuwasaidia watu wenye mahitaji maalumu hasa watoto yatima nchini.
Amesema mitandao ya kijamii inaumuhimu mkubwa ikiwa itatumika vizuri hivyo amewashauri wanajamii kutumia mitandao ya kijamii katika kuleta mabadiliko ya maendeleo nchini.
Mkurungezi wa Globify pia ni mjumbe maalumu wa Globify Charity Issa Halili Issa amesema mtandao huo ulianzishwa mwaka 2017 na umekuwa ukijihusisha na utoaji wa misaada mbali mbali kwa watoto yatima nchini ikiwa lengo ni kuonesha umuhimu wa matumizi mazuri ya mitandao ya kijamii ikiwa jamii itatumia mitandao vizuri itapelekea maendeleo katika nyanza zote nchini.
Katibu wa Globify Mectrida Chifungo amesema leo lupitia kituo hicho wamefanikiwa kukabidhi mchele,sukari,unga wa ngano na sembe,mafuta,taa za sola,magodoro,vijuzuu pamoja na mahitaji mengine ikiwa ni sehemu ya kuwasaidia watoto hao katika kuwatatulia baadhi ya changamoto na kuwafariji watoto hao kwa misingi ya kuwapa faraja na kujiona wana haki kama watoto wengine.
Akizungumza katika tukio hilo masaidizi msimamizi wa kituo cha kulelea watoto hao Thuwaiba Thabit amesema kituo hicho kina watoto 33 na kinajihusisha kulea watoto yatima na wenye mazingira magumu kwa watoto wa kike pekee na kupitia ujio wa ugeni huo wamefajika na kushukuru kwa msaada waliopatiwa kwani walikuwa na changamoto za ukosefu wa sola za taa hivyo wamewapongeza Globify kwa kitendo cha kuwajali na kuwathimini watoto hao.
Ametoa wito kwa taasisi mbali na jamii kwa ujumla nchini kuendelea kuwaona watu wneye mahitaji maalumu ili kuwapa faraja na kuwa nao pamoja katika hali zote.
Rayhanat Ridhwani Juma ni miongoni mwa watoto yatima wanao lelewa kituo hapo amewashukuru wageni kwa kuwafariji pamoja na msaada walioupata na amewaomba Globify usiwe mwisho wao wa kuwasidia watoto hao na watu wengine wenye mahitaji maalum.


