Popular services

SPIKA ZUBEIR:ATOA NENO KWA ZIPA, USALAMA NA AMANI CHACHU YA KUVUTIA WATALII NA WAWEKEZAJI KUJA NCHINI


Na,Nishan khamis:

Fukuchani W/Kaskazini A Unguja. 

Spika wa baraza la wawakilishi Zanzibar Mhe,Zubeir Ali Maulid, amesema uwepo wa usalama,amani na ushirikiano nchini ni chachu kubwa inayo wavutia watalii na wawwekezaji kuja kuekeza nchini jambo ambalo linapelekea kuongeza pato la taifa.

Mhe,Zubeir ameyasema hayo leo katika uzinduzi wa mradi wa  nyumba  za kulala wageni Moyo Mzuri Villa resort  zilizopo katika kijiji cha Fukuchani wilaya ya kaskazini A Unguja Mkoa wa Kaskazini Unguja ikiwa ni matunda ya maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya Zanzibar .

Aidha ameitaka Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar (ZIPA) ametaka  kufanya tathmini kwa Uwekezaji wa nyumba za biashara kwa wageni na kuishauri Serikali kwani wageni wengi wamekua wakipendelea kubakia Visiwani kwa muda mrefu Ili kukuza maendeleo katika sekta ya utalii nchini.

Spika ameseme Serikali imevutia Uwekezaji mkubwa katika sekta ya utalii kwani Idadi ya wageni inazidi kuongezeka na kufikia Wageni laki 6 na elfu  arobaini na imelenga  kufikia wagemi milioni 1 ifikapo mwaka 2030. 

Pia amesema kuwa asilia 37 ya miradi iliosajiliwa na ZIPA ni Miradi ya hoteli na 22 ni Miradi ya nyumba za biashara ambapo inaonesha Taaswira ya utalii inabadilika kwa Kasi ikubwa na hii imeachagiwa na amani pamoja na ukarimu kwa wakaazi wa Zanzibar.


Halikadhalika amewapongeza wawekezaji kuendelea kuwekeza nchini na amewahakikishia ikiwa yeye spika wa baraza atasimamia kwa weledi zaidi katika sera na sheria za Uwekezaji ila kuwavutia zaidi wawekezaji kuendelea kuja nchini na Zanzibar kuendelea kunufaika zaidi kiuchumi. 

Akitoa salamu za mkoa  Mkuu wa mkoa wa Kaskazini Unguja Mattar Zahor Masoud  amesema mradi huo ni wa 4 kati ya miradi 18 iliyopo katika mkoa huo inayoendelea kuzinduliwa katika mkoa huo ikiwa ni mafanikio ya mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964 ni vyema wananchi wakaendelea kuyaenzi na kuunga juhudi za serikali katika kuendelea kuimarisha miundoni kwa maendeleo ya taifa kwa ujumla. 

Mhe, Mattar amesema Uwekezaji unaendelea katika mkoa huo itasadia kwa kiasi kikubwa wananchi kunufaika katika upatikanaji wa ajira kwa vijana na kuendelea kuongeza pato na nchi huku akiwasisistiza wananchi kushirkiana na wawekezaji, serikali ya wilaya, mkoa na taifa kwa ujumla katika kuendeleza maendeleo ya nchi. 

Mkurugenzi Mtendaji Mamlaka ya Kukuza Uwekezaji Zanzibar ZIPA Saleh Saad Mohammed amebainisha kuwa ZIPA Ina jumla ya Miradi 424 yenye thamani ya Dolla  million 5.9 na inatarajiwa kutoa ajira 122  kwa vijana na kwa Mkowa wa Kaskazini Unguja Ina miradi 99 yenye thamani ya Dolla billioni 2.

Akizungumza katiaka ufunguzi wa mradi huo Muekezaji John Godson Mbwambo ameishukuru Serikali kupitia ZIPA kwa ushirikiano waliotoa na amesema Jumla ya vijana 33 wanatarajiwa kuajiriwa katika mradi wa kutoa  moyo ambapo hadi sasa tayari vijana 18 wameajiriwa 17 wakiwa wenyeji wa eneo Hilo na mmoja ni Mgeni.

Nao wananchi wa Fukuchani wamesema wamefurahishwa kuona vijana wazawa kupewa kipaumbe za ajira katika mradi huo huku wakiahidi kuendelea kutoa ushirikiano kwa wawekezaji na serikali kwa ujumla katika maendeleo ya nchi.