Popular services

MAPINDUZI CUP 2024/25 YATAHUSISHA TIMU ZA TAIFA BADALA YA VILABU.

Zanzibar. 

Kamati ya Kombe la Mapinduzi 2024/25, imetangaza rasmi Mashindano ya Kombe la Mapinduzi Msimu huu ambapo yatahusisha Timu za Taifa badala ya Timu za Vilabu kama ambavyo ilivyozoeleka tangu kuanzishwa kwa Mashindano hayo.

Akizungumza na Wandishi wa Habari, Makamo Mwenyekiti wa Kamati ya Mapinduzi Cup ambae pia ni Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Zanzibar ZFF Mahmoud Suleiman Jabir amesema kuwa Mwaka huu Mashindano hayo yatashirikisha Timu kutoka Mataifa sita ambayo ni pamoja na Zanzibar Heroes wenyeji wa Mashindano hayo, Kilimanjaro Stars, Kenya, Uganda Burundi na Bukinafaso.

Aidha Makamo Mwenyekiti amesema Mashindano hayo wamebadilishwa kwa Mwaka huu kutoka Vilabu na kuwa Mataifa ili kuzipa nafasi nzuri Timu zetu za taifa za Afrika Mashariki [Tanzania, Kenya na Uganda] kujianda na Michuano ya Chan ambayo inatarajiwa kufanyika mwezi Febuary.

Mashindano hayo ya Kombe la Mapinduzi 2025 ambapo ni Msimu wa 14 yanatarajiwa kuanza rasmi Januari 3, 2025 na kumalizika Januari 13, 2025. Mechi zote zitachezwa katika uwanja wa Gombani, Pemba huku Bingwa kuondoka na Milioni 100.