Popular services

MWAKILISHI ATOA NENO JUKWAA LA WANAWAKE VIJANA KASKAZINI UNGUJA.

 Na,Nishan khamis. 

Kaskazini Unguja. 

Mwakilishi  viti maalumu wanawake mkoa wa kaskazini Unguja Mhe,Mwanajuma Kasimu Makame amewataka wanawake mkoa huo kusimama imara katika mapambano dhidi ya vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia ndani ya mkoa na taifa kwa ujumla.

Ameyasema hayo leo huko Mahonda wilaya ya kaskazini B Unguja katika maadhimisho ya siku 16 za kupinga vitendo vya udhalilishaji yaliyo andaliwa na jukwa la vijana wanawake mkoa wa kaskazini Unguja.

Mhe,Mwanajuma amesema suala la udhalilishaji ni janga la taifa hivyo nguvu kubwa inahitajika kwa wanawake katika kujitathimini, kujiamini na kuacha masuala ya muhali katika kuondoa vitendo vya udhalilishaji katika mkoa huo.

Aidha amewapongeza jukwaa hilo kwa kuona jitihada wanavyo zifanya katika vita dhidi ya vitendo hivyo amewahidi kuendelea kuwa nao kwa hali na mali  huku akiwahamasisha kushirikiana na kuzikimbilia fursa za uongozi pamoja na kuchukua jitihada za kuwa na uwelewa wa rasilimali kwa wanawake. 

Aidha amewasisitiza kuwa mstari wa mbele katika kuhubiri kudumisha amani na upendo hasa kipindi tunacho elekea cha uchaguzi mkuu mwaka 2025 nchini 


Awali akimkaribisha mgeni rasmi katika hafla hiyo katibu wa jukwaa hilo Farihia  Abdallah Juma amesema jukwaa hilo limeanzishwa mwaka 2022 mpaka sasa linawanachama 36 wote wakiwa ni wanawake na malengo ya jukwaa ni kutoa elimu kwa wanawake kujiunga na jukwaa hilo kwa pamoja katika kupinga vitendo vya udhalilishaji wa kijinsia kwa wanawake na watoto,kujenga mashirikiano mazuri kwa wanawake na watoto wenye mahitaji maalum ambao ndio wahanga wakubwa wa matukio pamoja na kutoa ushauri kwa viongozi dhidi ya ushirikiano wa kuondoa vitendo hivyo. 

Mkurungezi wa Wasaidizi wa Sheria wilaya ya Kaskazini A Unguja Asia Fadhil Makame Akiwasilisha mada katika hafla hiyo alisema maadhimisho hayo ni ya  dunia nzima amabayo huanza November 25 na Disemba 10 kila mwaka hivyo kila mtu ananafasi ya kuhakikisha tunapinga na kuondoa vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia nchini. 


Asia amebainisha kuwa vitendo hivyo vina madhara makubwa nchini katika kurejesha nyuma maendeleo ya jamiii,huleta migogoro pamoja na kuathirika kiakili kwa wahanga wa matukio hayo,hivyo ni vyema serikali, asasi za kiraia na jamii kwa ujumla kuendelea kwa pamoja kuondoa vitendo hivyo.


Afisa kutoka dawati la jinsia Mahonda mkoa wa kaskazini Unguja Coplo Chum Makame Hemed amesema makosa ya udhalilishaji yamepungua kutoka mwaka 2023 makosa 162 hadi makosa 120 kwa mwaka 2024 ikiwa ni jitihada za serikali na taasisi mbali mbali kuendelea kutoa elimu juu ya madhara ya vitendo hivyo katika jamiii na taifa kwa ujumla ambapo ameeleza kwa sasa makosa yanayo jiri kwa wingi katika dawati la jinsia mkoa huo ni makosa ya udhalilishaji wa utelekezaji wa wanawake na watoto katika mkoa huo.


Hidaya  Rehani  Hassan akisoma risala katika hafla hiyo amesema licha ya jitihada wanazo zifanya jukwaa linakabiliwa na changamoto ya ukosefu wa ofisi rasmi pamoja na ukosefu wa mitaji mambo amabyo yanakwamisha kuto fanya kwa ufanisi utekelezaji wa majukumu yao kwa maslahi ya wanawake na watoto mkoa huo.