Popular services

WANAWAKE WAHIMIZWA KUZIKIMBILIA FURSA ZA UONGOZI PAMOJA NA UMILIKI WA RASILIMALI.


Na,Nishan khamis. 

Zanzibar. 

Mratibu wa shirika la Actionaid Zanzibar Bakar Khamis Bakar amewahimiza wanawaweke nchini kuzikimbilia fursa mbali mbali za uongozi zilizopo katika nyanza zote zikiwemo vyombo vya maamuzi pamoja na usimamizi wa rasilimali ili kuendelea kuleta uchechemuzi wa maendeleo kwa wanawake na usawa wa kijinsia nchini. 

Mratibu Bakar ameyasema hayo hapo jana  katika mjadala uliowakutanisha baadhi ya watendaji wa serikali,taasisi mbali mbali zisizo za kiserikali,wajumbe kutoka baraza la Wawakilishi Zanzibar,wadau na wanaharakati mbali mbali katika kuangazia hali ya ushiriki wa wanawake  katika masuala ya uwamuzi na usimamizi wa rasilimali kwa wanawake nchini mjadala huo ulio andaliwa na shirika la actionaid Zanzibar uliofanyika katika ukumbi wa mikutano hoteli ya Maru maru wilaya ya mjini Unguja. 

Amesema bado kuna changamoto za wanawake katika kuzikimbilia fursa za uongozi katika nyanza za kijamii, kiuchumi, kisiasa hivyo jamiii na taasisi mbali mbali ziendelee kushirikiana katika kuwahamasisha na kuwaunga mkono wanawake ili kufikia fursa za uongozi pamoja na umiliki wa rasilimali jambo ambalo limekuwa ni changamoto kwa baadhi ya wanawake Zanzibar katika utambuzi wa umiliki wa rasilimali. 

Akiwasilisha mada katika umjadala huo mkurungezi mtendaji wa taasisi PYI Rashid Mwinyi amesema licha ya jitihada za asasi na wadau mbali mbali kuendelea kuwahamasisha wanawake kuzikimbilia fursa za uongozi bado katika tatizo la wanawake kuzikimbilia fursa hizo na kuwapa nafasi kubwa wanaume kushikiria kwa asilimia kubwa nafasi za uongozi nchini. 

Rashid amesema kwa mujibu wa  takwimu zinaonesha wajumbe  baraza la wakilishi Zanzibar kwa upande wa wanawake ni viti 29 sawa na asilimia 37,wanaume viti 49 sawa na asilimia 63 ikiwa ni jumla ya viti 78 iwa vyote sawa na asilimia 100 ambapo kati ya viti 29 viti 8 ndivyo wanawake waliochanguliwa kupitia kura,viti 3 uteuzi wa rais na viti 18 uteuzi wa viti maalumu hali amabayo ni tofauti kubwa kwa upande wa wanaume katika nyadhifa izo.

Wadau mbali mbali wakitoa michango yao katika mjadala huo wamesema uwepo wa mifumo dume katika jamii,udhaifu wa baadhi ya sera ya vyama vya  siasa, baadhi ya sheria,ukosefu wa elimu ya uongozi ,uksoefu wa elimu ya rasimali fedha kwa wanawake, matendo ya udhalilishaji kwa wanawake  pamoja na uchumi duni kwa wanawake ni miongoni mwa mambo yanayo kwamisha ushiriki wa wanawake katika vyombo vya maamuzi pamoja na ushiriki mdogo katika kuzimbilia fursa za uongozi katila nyanza zote nchini.

Wamesema ili kuhakikisha mwanamke anashiriki ipasavyo katika kinyang'anyiro cha nafasi za uongozi nchini ni lazima mabadiliko yawepo katika baadhi ya sera ya vyama vya siasa,wawezeshwe kiuchumi wanawake, wapatiwe elimu ya uongozi itakayo wajenga kjiamini na kuweza kufikia malengo yao ya uongozi kwa misingi ya maendeleo ya usawa wa kijinsia katika utawlaa na nyadhifa zote.

Mkurungezi wa idara ya elimu msingi na awali kutoka wizara ya elimu na mafunzo ya Amali Zanzibar Fatma Mode akifunga mjada huo amesema ikiwa sheria na sera zitafuatwa ipasavyo zinaweza kuleta tija kwa wanawake kuzikimbilia fursa hizo nchini. 

Amesema serikali ya mapinduzi ya zanzibar inayoongozwa na Dkt Husein Ali Mwinyi imeleta mabadiliko makubwa katika kuwanyanyua wanawake katika uongozi na uchumi hali ambayo imeleta mabadiliko kwa wanawake nchini. 

Fatma amesema ushirikiano baina ya serikali, asasi zisizo za kiserikali na wadau mbali mbali ni vyema kushirikiana na kuibuka fikra kwa pamoja katika kusimamia kwa pamoja maendeleo ya wanawake na taifa kwa ujumla na kuendelea mapambano ya kutokomeza  vitendo vya udhalilishaji nchini. 


Aidha ametumia nafasi hiyo kuwaomba wazazi na walezi kufuatia kipindi hichi cha likizo kwa wanafunzi kuwa nao makini ili kuwalinda watoto dhidi ya vitendo vya udhalilishaji.