Popular services

SHAMSI AZINDUA SOKO LA KISASA MKWAJUNI ATOA NENO KWA WAFANYA BIASHARA


Na,Nishan khamis.
Mkwajuni Kaskazini Unguja.

Waziri kiongozi mstaafu wa serikali ya mapinduzi ya Zanzibar Mhe,Shamsi Vuai Nahodha leo amezindua soko la kisasa la mkwajuni wilaya ya kaskazini A mkoa wa kaskazini ikiwa ni shamra shamra za maadhimisho ya miaka 61 ya Mapinduzi ya mwaka 1964.

Mhe,Shamsi amesema serikali ya mapinduzi ya Zanzibar awamu ya nane inayoongozwa na rais Dkt Husein Ali Mwinyi imeipa heshima kubwa maono ya mapinduzi ya mwaka 1964 kwa kuimarisha maendeleo katika nyanza zote nchini yakiwemo ujezi wa masoko ya kisasa amabayo yemejengwa na yanaendelea kujengwa kwa kipindi kifupi cha madaraka ya Dkt Mwinyi ikiwa lengo kuwaekea mazingira rafiki na salama ya kibiashara kwa wafanya biashara kwa misingi ya maendeleo yao na taifa kwa ujumla.

Mhe,waziri kiongozi mstaafu amesema ujenzi wa soko hilo la kisasa ni ahadi ya Dkt Mwinyi katika ahadi zake ambazo amezitoa na ametekeleza kwa vitendo jambo ambalo wananchi wanatakiwa kumuunga mkono katika kuendeleza maendeleo zaidi nchini.

Aidha ametoa wito kwa kwa wakulima,wafugazi na wavuvi kulitumia soko hilo katika kuongeza kipato zaidi huku akiwataka baraza la manispaa na wafanya biashara  kulitunza soko na kutunza usafi muda wote ili kuepukana na maradhi mbali mbali yanayo tokana na uchafu ili kuweka haiba nzuri ya soko kwa maslahi ya wanafanya biasha kuwa salama kiafya na wananchi wote kwa ujumla.

Awali akisoma taarifa ya kitaalamu katibu mkuu wizara ya nchi afisi rais ,tawala za mikoa na idara maalum za SMZ ndugu Mikidadi Mbarouk Mzee amesema lengo kuanzishwa mradi huo ni kuondosha changamoto kwa wafanya biashara wote ambao hufanya biashara zao pembezoni mwa barabara ambapo soko hilo la kwa sasa limekamila kwa asilimia 100 kwa hatua ya mwanzo na shilingi Bilioni moja  milioni thelathini na tisa laki tatu hamsini nane elfu  na thelathini na mbili nukta mbili(Tshs 1,039,358,032.2/=) zimetumika kukamilisha ujenzi wa soko hilo.

Aidha amesema ujenzi wa eneo hilo lina ukubwa Square elfu saba,7000 utajumuisha jengo la wauza mabogamboga ndani yake kutakuwa na vizimba 144,maduka 11,jengo la wauza samaki na nyama kutakuwa na vizimba 32,cold room,vyoo vya matundu sita, mghawa na sehemu za kuewa magari, ambapo soko hilo litawahudumia wajasiriamali wasiopungua 400 hadi 500 kwa wakati mmoja.

Akitoa salamu za mkoa mkuu wa mkoa wa kaskazini Unguja Mhe,Mattar Zahor Masoud amesema kuendelea kuwepo kwa amani na utulivu nchini ni njia kubwa inayopelekea maendeleo na kuyaenzi Mapinduzi ya mwaka 1964 kwa kuimarisha amani,upendo na mshikanamo kama rais wa serikali ya mapinduzi ya zanzibar inayoongozwa na Dkt Husein Ali Mwinyi pamoja na rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt Samia Suluhu Hassan wanavyo hubiri kuendelea kutunza tunu ya amani nchini kwa maendeleo endelevu ya wananchi na taifa kwa ujumla.

Mhe, Mattar amesema uwepo wa soko hilo ni chachu ya maendeleo katika mkoa wake jambo ambalo amewataka wananchi kuchangamkia fursa hiyo kwa maslahi ya maendeleo ya mkoa na taifa kwa ujumla huku akiwahakikishia kupambana na wezi wa mazao na mifugo jambo ambalo ni changamoto kwa wakuli na wafugaji katika mkoa huo.


Nae mstahiki Meya baraza la Manispaa wilaya ya kaskazini A Unguja Machano Fadhil Machano(Babla) amesema kwa niaba madiwani,wafanyakazi wa Manispaa na wananchi kwa ujumla wanamshukuru rais Dkt Mwinyi kwa ujenzi wa soko hilo na miradi mbali mbali iiliyopo katika wilaya hiyo kutokana na utekelezaji wa wa vitendo kwa ahadi zake ikiwa anatekeleza ipasavyo ilani ya chama cha mapinduzi CCM kwa kuleta maendeleo ya wananchi wa Zanzibar ni jambo la kuungwa mkono kwa asilimia zote na fadhila zao ni kumrejesha tena madarakani katika uchanguzi mkuu 2025 kuendelea kuiongoza Zanzibar.